Friday, December 28, 2012
Thursday, December 27, 2012
KAZI IMEANZA….ILE RAP BATTLE YA CASSIDY NA MEEK MILL….HII NI KARATA YA KWANZA YA MEEK MILL…
Vita kati ya marapper wawili, Cassidy na Meek Mill wa Maybach tayari imeanza rasmi.
Baada ya juzi kati tu kujibizana kwenye twitter na kukubaliana kuingia kwenye rap battle…na hiyo ni baada ya mtu mzima Cassidy kuachia a diss track kwa Meek Mill “Me, Myself & iPhone”..sasa Meek Mill leo ameachia track yake ya kwanza kama diss kwa mtu mzima Cassidy.
Track inaitwa “Repo”….track ambayo Meek Mill amekwenda straight sana kwa mchizi bila kupindisha maneno na kuweka wazi changamoto anazokutana nazo kwenye game kutoka kwa marapper wa muda mrefu kidogo kama Cassidy…kwenye ngoma kuna lines anasema..” You talkin' 'bout a battle rap? How you gon' handle that? / Hundred grand pussy nigga? You ain't got the time for that / You ain't got the stacks for that / You know what we laughin' at,"
baaada ya hiyo picha ilioambatana na diss track ,cassady ali-tweet maneno haya ,,
Sikiliza track hiyo hapa.........
Chris Brown anajua kuwapanga Karuache Tran na Rihanna! Baada ya kula bata na Karuache kule Paris,Christmas hii alikuwa na Rihanna Los Angeles...
Pamoja na kwamba mpaka sasa Chris
Brown na Rihanna hawakubali kuwa wao ni
couples lakini matukio ya kuthibitisha hili yanazidi kuonekana.
Jana (december 25) katika
kusheherekea sikukuu ya Christmas star kutoka Barbados Rihanna mwenye miaka 24
aliamua kuchukua flight hadi Los Angeles ambako ali-join na Chris Brown
kushuhudia mechi ya mpira wa kikapu baina ya Lakers na Knicks iliyopigwa katika
uwanja wa Staples Center, Los Angeles
Marekani.
Ni kama wametoa picha yenye maelezo
kuwa wameamua kurudiana tena na kuendelea na maisha yao pamoja, na hii ni baada
ya Chris Brown kuonekana kuvuruga makubaliano yao hivi karibuni na kula bata na
mpenzi wake wa zamani Karuache Tran huko Paris Ufaransa, kitu ambacho kilimkera
sana Rihanna na kuandika tweet za matusi ambazo zilionekana kabisa kuwa
zilielekezwa kwa Chris Breezy kwa kukutana tena na Karrueche Tran wakati huo
Rihanna yuko mpweke kwenye mapumziko yake akitegemea ujio wa Chris Brown.
Chris Brown na RiRi walionekana
wenye furaha sana wakitabasamu na kucheka mara kwa mara wakati wanaangalia
mechi ya Lakers siku hiyo ya Christmas huko Los Angeles. Ni kama Chris Brown
anaweza kuwamudu na kuwacontrol warembo hawa wawili matata.
Baada ya game kuisha RiRi alitweet picha
aliyopiga na Chris Brown wakiwa wamepose katika Porshe 911 Turbo S
aliyozawadiwa na lebel yake ya Roc Nation ya mtu mzima Jay Z hivi karibuni, na
picha hiyo ilikuwa na caption iliyosomeka "Thug Life, Merry
Christmas".
DAN ROCK FEAT. AT - KITOLA OFFICIAL VIDEO FULL HD
Official Video ya msanii DAN ROCK feat. AT. Nyimbo inaitwa KITOLA na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri
Wednesday, December 26, 2012
WIZ KHALIFA NA 50 CENT KUFANYA MOVIE PAMOJA....
Baada kutoka na film ya Mac & Devin Go To High School akiwa na Snoop Dogg ,Wiz Khalifa amenogewa na biashara hiyo na sasa yupo kwenye mipango ya kutengeneza movie nyingine ambayo itamshirikisha star wa rap ,
Akipiga story na DJ Whoo Kid ,wiz amedhibitisha kuwa alizungumza na 50 Cent juu ya kufanya movie na soundtrack pamoja , “ nilikuwa na 50 Vegas na tukazungumza juu ya kutengeza movie na soundtrack pamoja . “nataka niwe drug dealer kwenye hiyo movie. Nataka nishike pistol. Akatania ,Nataka niwashoot ,”
Check out interview yake na DJ Whoo Kid , Wiz anazungumzia ujauzito alionao Amber Rose, na kwanini snoop or Curren$y hawajatokelezea kwenye albam yake, na anasubiri kufanya kazi Dr. Dre,
Tuesday, December 25, 2012
TAARIFA KUTOKA JWTZ: WATAMCHUKULIA HATUA KALI MWANAJESHI ALIEPIGA PICHA NA LEMA,
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona
taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya
Monduli, Arusha, iliyochapishwa katika gazeti la Mwanandhi la Desemba
24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.
Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.
Ilikuwa rahisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu.
Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.
Ilikuwa rahisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu.
Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga
MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga
source:http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/373747-tamko-la-jwtz-juu-ya-picha-ya-lema-na-mwanajeshi-katika-mwananchi-la-leo.html
Monday, December 24, 2012
RIHANNA AICHANGIA HOSPITAL YA KWAO BARBADOS DOLA 1.75 MIL ILI KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KANSA…..
Baaada ya mafanikio ambayo bado
anaendelea kuyapata siku hadi siku…Rihanna aichangia kiasi cha dola 1.75
milioni hospitali ya huko kwao Barbados.
E! News imeripoti kuwa R&B Diva
Rihanna ametoka kiasi hicho kama kumbukumbu ya marehemu bibi yake Clara “Dolly”
Braithwaite ambaye alifariki kutokana na kansa mwezi June mwaka huu.
Mchango huo umeelekezwa kwenye idara
ya ‘rediotherapy’ katika hospitali ya Queen Elizabeth iliyoko Bridgetown huko
Barbados na hiyo idara inatakiwa iitwe ‘Clara Braithwaite Centre for Oncology
and Nuclear Medicine’
“Hii ni njia yangu ya kurudisha
Barbados..kwa namna ya ‘philanthropy’..kwa kusaidia muendelezo wa mpango huu wa
kisasa…na naamini hii itakuwa na faida kubwa sana kwa watu wa Barbados…itaokoa
maisha na kuwafanya waishi muda mrefu zaidi”….amesema Rihanna.
DRAKE AMUOMBA JAJI KUTUPILIA MBALI SHAURI LA KESI YA KUPIGANA CHUPA CLUB NA CHRIS BROWN…..
Japokuwa yeye mwenye Drake alikuwepo….na
inawezekana akawa ni sehemu ya kilichotokea kwenye ugonvi ndani ya nightclub
baina yake na Chris Brown…lakini anaamini ahusiki na muonekano mbaya wa W.i.P.
nightclub kwa jamii kwa sasa.
TMZ imeripoti kuwa Drake amemuomba
jaji alitupilie mbali shauri hilo hata kama urushwaji wa chupa ulianza baada ya
Drizzy na Chris Brown walianza kurushiana chupa.
Na katika kukandamizia hilo Drake
amesema hata ‘New York Times’ magazine limeandika kuwa club hiyo imekuwa na
historia ya fujo na matatizo mengine.
Club hiyo ‘W.i.P. Nightclub’
ilifungwa mwaka 2011 na NYPD (mamlaka) na siku za nyuma ilishawahi
kusimamishiwa kibali chake kutokana na matukio ya fujo kufululiza kwa muda
mrefu.
Nyakati fulani Chris Brown aktika
moja ya interviews zake aliwahi kukataa kuizungumzia ishu hiyo kwa sababu
tayari ilikuwa kwenye vyombo vya kisheria…
Saturday, December 22, 2012
RAPPER FAT JOE HUENDA AKAENDA JELA MIAKA MIWILI KWA KUKWEPA KULIPA KODI...
Rapper Fat Joe ameshitakiwa na serikali ya marekani kwa kosa la kukwepa
kulipa kodi,
Fat Joe au Joseph Cartagena mwenye umri wa miaka 42 anafahamika kwa kazi alizowahi kuzifanya late Big Pun, Terror Squad na wakali wengine kibao, amepatishwa kizimbani katika mahakama ya New Jersey,na uhenda akashitakiwa miaka miwili jela lakini kwasasa yupo nje kwa dhamani ya $250,000,
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa April mwakani .
Fat Joe au Joseph Cartagena mwenye umri wa miaka 42 anafahamika kwa kazi alizowahi kuzifanya late Big Pun, Terror Squad na wakali wengine kibao, amepatishwa kizimbani katika mahakama ya New Jersey,na uhenda akashitakiwa miaka miwili jela lakini kwasasa yupo nje kwa dhamani ya $250,000,
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa April mwakani .
Friday, December 21, 2012
LULU AACHIWA KWA DHAMANA
Na Prince Akbar
MAHAKAMA Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, leo asubuhi imemuachia kwa dhamana msanii wa filamu
nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayetuhumiwa kumuua msanii
mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ baada ya kupitia vifungu vya sheria.
Hatua hiyo
inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kubadilisha mashitaka ya
mwanadada huyo kutoka kesi ya mauaji hadi kuua bila kukusudia.
Kutokana na
mabadiliko hayo, hata kama atashindwa kesi, Lulu hatapewa hukumu ya kunyongwa
kwa kuwa anatuhumiwa kwa kesi ya kuua bila kukusudia na kwa mujibu wa kifungu
cha sheria, anaweza kufungwa maisha au miaka kadhaa.
Lulu anakabiliwa
na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu
nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam.
Lulu
aliyecheza filamu kadhaa na marehemu Kanumba waliyeibuka naye katika kundi la
Kaole, Magomeni, anadaiwa alimsukuma Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican, ambaye
pia inadaiwa alikuwa mpenzi wake.
Inaelezwa
baada ya tukio hilo, Lulu alikimbia nyumbani kwa Kanumba na mdogo wa The Great,
Sethi Bosco akaenda kuchukua gari kumpeleka kaka yake hospitali ya Muhimbili,
ambako alipofika iligundulika amekwishafariki dunia.
Sethi
alikaririwa akisema kwamba siku ya tukio, Lulu alikwenda kwao usiku wa manane
na alipofika yeye (Sethi) alimuacha aongee na kaka yake. Sethi alidai aliwaacha
sebuleni akaingia chumbani kwake na baadaye akasikia wameingia chumbani (kwa
Kanumba).
Sethi
alisema baada ya muda alisikia kelele za dalili ya ugomvi na baada ya muda Lulu
alitoka kumwambia (Sethi) juu ya hali ya Kanumba kubadilika na kuwa mbaya.
Sethi alidai
aliposikia hivyo akashituka na kwenda chumbani ambako alimkuta kaka yake katika
hali mbaya, povu likimtoka mdomoni hivyo kuchukua hatua ya kumuita daktari
wake, kabla ya kumkimbiza Muhimbili.
Lulu
alikamatwa asubuhi ya kuamkia siku ya tukio hilo, linalodaiwa kutokea usiku wa
manane na kuwekwa kizuizini katika kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar
es Salaam, kabla ya kufikishwa mahakamani.
Uchunguzi wa
madaktari katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ulisema pombe kali aina ya
Jackie Daniels ilisababisha kifo cha mwigizaji huyo.
Kifo cha
Kanumba kiliwaumiza wengi, kwani msanii huyo alikuwa mahiri na kipenzi cha
wapenzi wa filamu nchini.
Wapembuzi wa
mambo wanasema huu ni msiba wa kwanza kuteka hisia za watu wengi zaidi, tangu
kifo cha baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba mwaka 1999.
RIHHANA APOKEA GARI LA KIFAHARI KAMA ZAWADI YA XMAS KUTOKA KWA JAY Z...
zawadi ya Xmas aliyopewa Rihana- a brand new Porsche 911 Turbo S Kutoka kwa rap mogul, Jay-Z akishirikiana na utawala mzima wa label ya Roc Nation.gari hii anagharama ya $200,000.
MBUNGE KABATI ATOKA NA WIMBO WA MKALI NA TOP 2O YA KABATI STAR SEARCH ...
Mbunge wa viti maalum (CCM) Ritta Kabati akiingiza mashairi katika wimbo
mpya akishirikiana na vijana chupikizi 20 wa kabati star search katika
studio za Top Magic Sound zilizoko Ipogoro Iringa mjini.
Na Denis Mlowe – Iringa
Muziki wa kizazi kipya
wengi wanaujua kama bongo fleva wazidi kuwavutia viongozi mbalimbali na wengine
wanaimba hadi sasa kama Joseph Mbilinyi aka Sugu, Vick Kamata sasa amejitokeza
mbunge mwengine wa viti maalum toka chama cha mapinduzi Ritta Kabati na
kuufanya uwe gumzo katika maisha ya watanzania na nchi za jirani kitu
kinachofanya watu mbalimbali kujitokeza kuupenda na wengine kuamua kuingia kwa
kasi katika tasnia hii ya burudani Tanzania.
Katika kuukuza zaidi
muziki huu Mbunge wa Viti maalum kupita chama cha Mapinduzi mkoani Iringa Ritta
Kabati akishirikiana na wasanii chipukizi 20 wa kwanza waliotokana na shindano
la kutafuta vipaji la Kabati Katiba Star Search amefanikiwa kutoka wimbo mmoja
unaokwenda kwa jina la 'Iringa Bila Ukimwi Inawezakana' uliofanywa katika
studio za Top Magic Sound chini ya mzalishaji anayekuja kwa kasi pande za
Nyanda za juu Kusini Ecko Msigwa.
Wimbo huo ni harakati
za mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga kama
uvutaji wa bangi, kuepukana na maambukizi ya ukimwi katika mkoa huu ambao
unaongoza kwa sasa nchini Tanzania na amesema kwamba wakati anafikiria kuingiza
mashairi hayo kwa kweli alikuwa katika hali ya huzini kwa jinsi vijana
walivyoweza kufanya vizuri katika wimbo huo kwa lengo la kuwakomboa watanzania
kupitia muziki.
Baadhi ya mashairi ya
hayo ni ‘ndugu zangu watanzania nina maumivu makali sana, tumepoteza ndugu
zetu, jamaa zetu na marafiki zetu dira ya maendeleo inateketea ni wakati wetu
kupambana iringa bila ukimwi inawezekana’ “ kwa kweli nina uhakika wa
kuwafunika vijana hawa katika wimbo huu ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na
wakazi wa mkoa huu kwa kuwa ni mkusanyiko wa vipaji vya kweli vilivyotokana na
shindano nililoandaa” alisema Kabati
Wimbo huo unatarajia
kuzinduliwa rasmi leo katika radio zote za Nyanda za Juu Kusini na kisha
kusambazwa katika radio zote nchini Tanzania na amewataka wadau kuwapa nguvu
vipaji hivi kwa kununua kazi za vijana kwa lengo la kuwaongeza kipato na
kuondoka na maisha ya vijiweni.
@kwa hisani ya francisgodwin.blogspot.com
“NIGGAZ IN PARIS” YA JAY Z NA KANYE WEST YATAWAZWA TRIPLE PLATINUM…
Ni mwaka tayari umekatika tangu
Kanye West na Jay Z waiachie kitaani albam yao ya pamoja…”Watch The
Throne”…albam ambayo mpaka hivi sasa imeshanyakuwa tuzo kibao sana…ambayo kadri
muda unavyozidi kusonga ndivyo tracks ndani ya mzigo zinavyozidi kushika zaidi.
Kwa mujibu wa HHNM…”Niggaz in Paris”
moja kati ya ngoma makini sana zinazopatikana kwenye albam hiyo tayari
imetawazwa triple platinum baada ya kufikisha mauzo ya nakala milioni 3.
Mafanikio ya baadhi ya ngoma kutoka
ndani ya albam hiyo hayajaishia hapo coz ngoma “No Church in the Wild” ambayo
Frank Ocean amenyonga choras flani matata pia imetawazwa GOLD..tayari imekuwa
ikitumika kwenye matangazo ya magari, movies na bidhaa zingine kibao.
“Niggaz in Paris” ni ngoma Jay Z na
Kanye wanaitegemea sana kwenye kuamsha watu mara zote wanapokuwa kwenye
concerts mbalimbali…na mara nyingi wamekuwa wakii-perform zaidi ya mara saba
kwenye tamasha moja kutokana na maombi ya fans...
T.I AZUNGUMZIA ALIVYOM’SIGN MEEK MILL GRAND HUSTLE….NI SEHEMU YA SAFARI YA MEEK MILL KIMUZIKI….
Kabla hajawa rapper anayefahamika
sana kama ilivyo sasa chini ya Maybach Music lebel…mtu mzima Meek Mill alikuwa
amesign kwa muda mfupi na Grand Hustle Records ya T.I.
Akipiga interview na Power 99 fm ya
Philadelphia..bosi wa zamani wa rapper huyo na mfalme kutoka South..mtu mzima
T.I amezungumzia mwanzo wa Meek Mill pale Grand Hustle.
Tip amesema bado anahisi kubeba
majuto ya haja kwa kumwachia Meek Mill aondoke…lakini pamoja na hayo yote
anajivunia mafaniko ya mchizi huyo kwa sasa akiwa na lebel nyingine.
“Mimi na Meek Mill tulikuwa pamoja
awali Grand Hustle..kutokana na mambo ya hapa na pale yaliyokuwa yananizunguka
kwa wakati ule sikuweza kufanya chochote kwa yeyote…na ndicho kilichomfanya
aondoke na kwenda kwa Rozay…japo nilikuwa na mkataba naye lakini sikuona maana
ya mimi kumzuia wakati sikuwa na uwezo wa ku’match na situation yake…bado
nilikuwa hata nikirudi nyumbani ninakuwa mambo mengi sana ya kufanya…so kama
uamuzi wa kwenda MMG ulikuwa ni uamuzi mzuri kwake sikuona namna ya kulizuia
hilo”…amesema T.I
Akaongeza..”Ninafurahia mafanikio
yake…kiukweli kabisa…na najisikia kama nami ningehusika kwenye mafanikio hayo
ingekuwa mzuka sana…mwisho wa siku maisha ndivyo yalivyo…wakati mwingine
hakitokei kile unachotaka kitokee”.
Subscribe to:
Posts (Atom)




















