Friday, December 21, 2012

#BARUA ALIOANDIKA RIHANNA KWENDA KWA FANS WAKE

0 comments
Baada ya  Beyonce sasa ni zangu ya Rihanna kuandika barua kwa mkono kwenda kwa fans wake .
kufuatia  kufanya vizuri kwa albam yake Unapologetic pamoja na 777 tour, Rihanna ameandika barua kwa mkono na  amei-adress barua hiyo kwa Navy, akikumbushia safari yake katika  musiki


“ miaka 7 albam 7 nikitu kikubwa cha kufurahia ,kumbukumbu nyingi za furaha na bado tupo pamoja safarini ,tumetengeneza habari mpya ,tukashare vicheko,tumekutana na watu wapya,tukapiga story ,kwa imani na matumaini” ameandika Ri Ri katika sehemu ya barua hiyo”
 #soma barua hiyo hapa
 




Wednesday, December 19, 2012

KUTOKA FACEBOOK# LUDACRIS.....

0 comments

T.I ASEMA..JAY Z ALITAKIWA AWEMO KWENYE “TROUBLE MAN: HEAVY IS THE HEAD”……..

0 comments
 

Baada ya kucheleweshwa kwa miezi kadhaa…mzigo wa mtu mzima T.I “Trouble Man: Heavy is the Head” hatimaye uko kitaa hivi sasa…akipiga interview na XXL Magazine…mfalme huyu toka South anayemiliki lebel ya Grand Hustle Records amezungumzia collabo ambayo aliipanga iwemo lakini alishindwa kuikamilisha kwenye mzigo wake huu wa nane.

Kwa mujibu wa T.I mwenyewe ni kwamba mtu mzima Jay Z alitakiwa aingie kwenye mkono unaitwa “G Season” lakini ikashindikana na badala yake akaingia bwana mdogo aliye chini ya MMG…Meek Mill na kuweka verse kwenye beat ya ngoma hiyo iliyotengenezwa na Cardiak.

“Nilimuomba Jay Z aingie kwenye ngoma hiyo…najua jamaa yuko tyt sana na mambo kibao anayoyafanya…na baada ya kushindikana nikamkamata Meek Mill…tulikuwa kwenye shughuli flani hivi ya Kanye West…nikamwambia…’mwana kuna kazi moja naomba unisaidie’..tukatoka tukaenda sehemu tukapata msosi then tukadondoka kwa studio ya Just Blaze huko Harlem na tukamaliza mzigo.”…amemaliza mtu mzima T.I.

Alicia Keys ashitakiwa kwa kuiba mistari ya mashairi ya hit song yake “Girl on Fire”.

0 comments

R&B diva Alicia Keys amekumbwa na msala wa kesi inayohusiana na kuvunja sheria ya hakimiliki, yaani copyright infringement kwa kunakili bila ruhusa ya mmiliki baadhi ya mistari inayosikika kwenye wimbo wake akiwa na Nicki Minaj ‘Girl on Fire’.
Keys anashtakiwa na mwandishi wa nyimbo anaeitwa Earl Shuman ambae anadai kuwa Alicia Keys aliiba mistari miwili kwenye wimbo unaoitwa “Lonely Boy” ambao aliandika akishirikiana na mwanamuziki Leon Carr na kurekodiwa na Eddie Holman kwa jina la “Hey There Lonely Girl” mwaka 1970 na ikashika nafasi ya pili kwenye Billboard chats enzi hizo.
 
Kwa mujibu wa blog ya blogger maarufu Friedman, Alicia Keys alitumia sekunde mbili tu za kwenye wimbo halisi aliokopi lakini ndizo zilizomsaidia kurekodi wimbo wake mzima wa ‘Girl on Fire.’
Mwandishi huyo mkongwe katika sanaa ya uandishi wa nyimbo ambao kwa wenzetu walioendelea wanauheshimu sana ametoa ripoti kupitia blog ya Friedman (show bizz 411) kuwa ameshafungua kesi mahakamani akimshtaki Alicia Keys, kampuni ya Sony Music waandishi Salaam Remi na Billy Kravan ambao wamehusika pia kuandika “Girl On Fire”. Katika mashtaka hayo Shuman ameeleza kuwa mshitakiwa(Alicia Keys) amevunja sheria kwa kuingilia hakimiliki yake kwa hiyo anahitaji fidia ya kazi yake, ikiwa ni pamoja na faida iliyopatikana kwenye wimbo huo “Girl on Fire.”
Wakati mrembo huyo anahitajika kujibu mashtaka mahakamani, yeye anaendeleza mashambulizi ya kuumaliza mwaka na vitu vikali na ameachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa “Brand New Me” ambayo iko kwenye album yake ya “Girl on Fire”
Haya mambo yangekuwa yana exist hapa kwetu nadhani kuna wasanii wengi sana wangekuwa  wanapishana mahakamani sababu iko list ndefu sana, na kazi za watu wengine zingeheshimiwa.

MAPENZI YA PREZZO NA GOLDIE KATIKA LEVEL ZINGINE...

0 comments

Mapenzi ya wakali wawili kutoka Africa Kenyan bad boy Prezzo na Nigerian singer Goldie, ambao walikutana kwenye  Big Brother AfricaStargame,yamekuwa yakipiga hatua  siku baada ya siku….

Si muda mrefu tangu Prezzo  kuamishia maisha yake nchini Nigeria kwasababu ya Goldie. Kupitia  press conference alioifanya hivi karibuni  Prezzo amekubali kuwa na mapenzi ya dhati kwa  Goldie  na akakili  kuwepo uwezekano wa kufunga ndoa…

Na kwasasa Prezzo  ameyapeleka mapenzi yake na Goldie kwenye  twitter, sehemu ambayo sio ngeni katika mapenzi yao..

CHECK TWEET  ZAO

Wsup Prezz? What’s the time? Ace♠” Goldie tweeted at Prezzo.

Prezzo tweeted back and called Goldie first lady, “It’s time 2 shine & make em fall in line, 1st lady!” Prezzo replied.

Ur the bestest and I am the luckiest, stay on ur grind and let nothing or no one put u dwn coz ur a star #24K all day errday, Prezzo, ambaye ni balozi wa  One Campaign panoja na  JayZ hiyo ndo tweet yake ya mwisho kwa Goldie  jana…

Goldie na  Prezzo  wamekuwa wakihudhulia events tofauti tofauti pamoja, Kenya na nje ya Kenya….

 

Tuesday, December 18, 2012

BUSTA RHYMES KUDROP A NEW MIXTAPE MWEZI HUU…INAITWA “CATASTROPHIC”….

0 comments
Akiwa chini ya muhuri wa lebel ya YMCMB…mtu mzima Busta Rhymes aka Basta Buss ametangazwa kudrop na mixtape mpyaaaa kabisa mwezi huu-huu.
Albam ya mwisho ya mtu mzima huyu ni “Year of The Dragon” ambayo rasmi ilidondoka mtaani mwezi Aug na akaonekana yuko kimya dizain.
Sasa inavyoonekana ni Holiday hii ni kama imemkurupua…ambapo mixtape kwa jina la “Catastrophic” itaingia mtaani Ijumaa ya Dec 21…mixtape ambayo inasemekana itakuwa chini ya The Conglomerate Ent. Na Shaheem Reid…kitaalamu kwenye cover imeandikwa Conglomerate project, featuring Busta, J Doe and Reek Da Villian.

2 CHAINZ ATANGAZA RASMI “B.O.A.T.S” KUTAWAZWA GOLD…….

0 comments
Akizivunja habari hizi kupitia Twitter…mtu mzima 2 Chainz aka Tity Boi amesema mzigo wake “Based on A T.R.U Story” mpaka sasa umeuza nakala zaidi ya 500,000 hivyo kutawazwa rasmi ‘GOLD’..na kuwashukuru wale wote waliowezesha hilo.
Tweet yake ilisomeka “Namshukuru Mungu, familia, timu, mashabiki, dj’z, taste makers, bloggers na wewe pia kwa support…tupo GOLD tayari…#Basedonatrustory(B.O.A.T.S.)#”…
“Based On A T.R.U Story” aka B.O.A.T.S. rasmi ilidondoka mtaani Aug 14, 2012 na moja kwa moja ikafika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Top 200 Albams kwa kuuzwa nakala 147,000 wiki yake ya kwanza tu.

Nazizi ANUSULIKA KUUMIZWA KATIKA TUKIO LILOHUSISHA RISASI

0 comments
Weekend iliyoisha  rapper and reggae singer Nazizi Hirji aliuhusika katika tukio la risasi lililotokea nchini humo kwenye bar ndogo iitwayo Calypso bar iliyopo Cannon Towers , Mombasa na inauwezo wa kuchukua watu kama 15  tu..
Kwamujibu wa Naziz nikwamba jamaa mwenye bunduki mkononi aliiteka bar hiyo akitafuta kundi la watu ambao wali mpiga na kumuachia  na majeraha,inadaiwa yalitokea mabishano nje  kabla ya jamaa kuiteka counter na kimimina risasi kwenye grass na chupa,
Baada ya mua mmfupi police waliwasili na kumkamata na kugundua kuwa jamaa alikuwa katika bar hiyo akiwatafuta wabaya wake walio mpiga na kumuachia majeraha makubwa
 Hata hivyo Kenyan post wameripoti kuwa hakuna hata raia alie pata madhara katika tukio hilo..

NAZIZI PIA KUTOKA NA ALBUM ,January

Nazizi Hirji ambaye ni Former member wa  Necessary Noize  anatarajia kutoka na albam yake January mwakani albam ambayo amerecord na mkali wa dancehall kutoka   Jamaica Ginjah.

   
                                                         Ginjah.
Nazizi anasema amekwisha kumaliza kutengeneza albam na Ginjah kupitia recording label kutoka  Italia ambayo wamesign nayo kwa usambazaji wa mzigo huo.
album imepangwa kuzinduliwa rasmi nchini Kenya na kufuatiwa na kabla ya kwenda kufanya tour barani ulaya  , Nazizi ameondoka Nairobi na kwenda  Malindi ilikuelekeza mawazo yake katika familia yake  na kwasasa yupo katika tour huko Mombasa na  Warriors From the East, band kutoka  Arusha