Nchi ya Nigeria ndio inayoongoza kwa kuwa na wachezaji wengi katika ligi ya NBA hadi
sasa,
Orodha hii inahusisha wachezaji ambao wanacheza kwa sasa katika
timu mbalimbali ndani ya ligi hiyo ya NBA.
Hasheem Thabeet
Taifa: Tanzanian
Urefu: 7 ft 3 in
Thabeet siyo mgeni katika mchezo huu wa kikapu ingawa ameingia
akiwa amechelewa, ameanza kukiendeleza kipaji chake baada ya kuwa kuanza
kuangalia mashindano mbalimbali jijini Dar es Salaam. Amehudhuria katika Chuo
Kikuu cha Connecticut. Mwaka 2008 na 2009 amewahi kutajwa kuwa mchezaji wa
mwaka na NABC kama mlinzi bora wa mwaka.
Ni mtanzania wa kwanza kucheza katika
lihi hii ya NBA kutajwa kuchezea timu ya Memphis Grizzlies mwaka 2009. Baadaye
akachezea timu za Houston Rockets na Portland Trail Blazers kabla hajaenda
katika timu ya sasa ya Oklahoma City Thunder. Thabeet ni mchezaji mrefu zaidi
katika wachezaji wa NBA. Mwezi November mwaka huu Thabeet ameweka rekodi yake
ya kwanza katika mchezo huo kwa double-double akiwa na pointi 13 na rebound 10.
Festus Ezeli
Taifa: Nigeria
Urefu: 6 ft 11 in
Ezeli ametumia muda wake mwingi wa utotoni katika masomo akiwa
kwao nchini Nigeria. Ni baada ya kuanza kuishi na mjomba wake nchini Marekani
ndipo alipoanza kucheza kikapu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 14. Mara ya
kwanza kuingia katika mchezo ilikuwa ni kama ajali baada ya kutofahamu na
kujikuta akifunga katika goli lake. Ni mwaka 2006 ambapo mwishowe alianza kukaa
vizuri katika mchezo huo na mwezi July mwaka 2007 alipata mwaliko kutoka Reebok
All-American Camp.
Wakati huo alikuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt
kwa miaka mitatu kabla hajakuwa nyota katika mchezo huo wa kikapu, akiwa na
wastani wa pointi 13 na rebound 6.3. msimu huo aliyajwa kuwa namba mbili katika
timu ya All-SEC (Southeastern Conference). Kwa sasa anakipiga katika timu ya The
Golden State Warriors akiwa na umri wa miaka 23 na amesajiliwa na timu hiyo
mwaka huu wa 2012.
DeSagana Diop
Taifa: Senegal
Urefu: 7 ft 0 in
Diop amekulia nchini kwao Senegal, ambako alikuwa anapenda
kucheza mpira wa miguu. Ameanza kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 15.
Alijiunga na masomo ya sekondari katika shule iliyoitwa Oak Hill Academy mjini Virginia,
ambako alikuwa anawaongoza kwa kushika namba moja katika orodha ya taifa. Diop alitajwa
kujiunga na timu ya Cleveland Cavaliers moja kwa moja akitokea shuleni.
Amedumu
kwa misimu minne akiwa na timu ya Cleveland kabla ya kutimkia timu ya Dallas
Mavericks, New Jersey Nets kisha Charlotte Bobcats mwaka 2009 ambako anakipiga
hadi sasa. Diop, ambaye ana uwezo wa kuzungumza lugha tano, ni muislamu. Ana
akaunti katika mtandao wa mawasiliano ya kijamii wa twitter ambao huutumia
kuelezea kuhusu maisha yake hasa watoto wake.
Al-Farouq Aminu
Taifa: America/Nigeria (huiwakilisha nchi ya Nigeria katika
mashindano ya kimataifa)
Urefu: 6 ft 9 in
Aminu amepata elimu yake katika shule ya Norcross High School, Georgia
shule ambayo hujulikana zaidi kuzalisha wanamichezo. Kibongo bongo hapo ni
Makongo. Alikuwa anaiongoza timu ya shule katika kushinda mashindano mbalimbali
na amewahi kucheza katika timu ya McDonald's All-American Team. Akiwa chuo
alikuwa anachezea Wake Forest.
Wakati akiwa chuoni mwaka 2009 alikuwa katika
timu ya Sporting News All-Freshman. Mwaka 2010 alikuwa chaguo la nane la timu
ya LA Clippers. Mwaka 2011 aliuzwa katika timu ya New Orleans Hornets ambako
anacheza hadi sasa. Ameichezea timu ya taifa ya Nigeria katika mashindano ya
Olympic mwaka 2012.
Bismack Biyombo
Taifa: Congo
Urefu: 6 ft 9 in
Biyombo amegundulika katika mashindano ya vijana yaliyofanyika
nchini Yemen wakati huo akiwa na umri wa miaka 16. Ugunduzi wa kipaji chake
ukamuongoza kucheza na mhispania Illescas, ambapo aliitwa kuchezea timu ya
wakubwa.
Akadhihirisha kuwa ni mchezaji wa kimataifa kwa timu ya Fuenlabrada.
Biyombo aliufanya ulimwengu wote kumtupia macho hasa wale wanaotafuta wachezaji
baada ya kuweka rekodi ya kwanza katika kikapu ya triple double (akiwa na
pointi 12, rebound 11 na block 10) katika mashindano ya 2011 Nike Hoops Summit.
Baadaye mwaka huo huo wa 2011 alichaguliwa kuichezea timu ya Sacramento Kings, lakini
akauzwa kwenda timu ya Charlotte Bobcats, ambako anakipiga hadi sasa.
Christian Eyenga
Taifa: Congo
Urefu: 6 ft 7 in
Eyenega alianza kuichezea timu ya kikapu ya nyumbani kwao Congo
katika timu ya Onatra Kinshasa. Na haichukua muda mrefu akatimkia nchini
Hispania wakati huo akiwa na umri wa miaka 17 na akafanikiwa kujiunga na timu
ya DKV Joventut. Baadaye Eyenga akabounce kati ya timu ya Prat na DKV Joventut.
Mwaka 2010 aliichezea timu ya Cleveland Cavaliers, mara ya kwanza katika ligi
kuu ya NBA kasha akafanya mkataba wa miaka miwili uliokuwa na thamani ya dola 2
million.
0 comments:
Post a Comment