Saturday, August 24, 2013

KAMIKAZE:MAPRODUCER WA BONGO WATAFUTE UTAMBULISHO WA MUZIKI WETU 'IDENTITY'

http://baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2013/03/cyril.jpg

Cyrill aka Kamikaze ambaye kwasasa ametambulisha track mpya ‘’FUMBA MACHO’’ft Dulayo amesema sababu za wasanii wa kenya na uganda kupiga hatua katika muziki tofauti na watanzania ni kutokana na kuwa na utambulisho wa kipekee katika kazi zao..

 Kutokana na kuliona hilo Kamikaze amewataka maproducer kutafuta utambulisho wa muziki wa tanzania (identity )

Nikimnukuu akipiga story na swahiliInfo. Amesema’’maproducer wangekaa chini wajaribu  kutafuta test yetu sisi watanzania ,unajua ukisikia mdundo flani unajua huyu Nigeria hata uimbaji wao ,unajua ,lakini leo hii nikifanya hivyo utasikia kwanini umehama ,sisi waganda wakenya wanatupita why?tuna miaka mingi tangu tumeanza muziki wetu saivi tunaweza tukahesabu miaka 16 au 17 ya muziki wetu lakini hatujasogea hata step moja huwezi amini .kwasabu hatutaki kukubaliana na ukweli ,hatutaki kukubaliana na market inavyokwenda ,bado tunataka tufanye  muziki ambao tutasifiana tu dah!jamaa umeandika una punchlines kali na unasema unataka uende nje uende Nigeria uende south Africa uende wapi utambulike kimataifa alafu unapita kwenye mdundo kama unaopita Rick Ross its so good kufanya hivyo bt to me nazani ni vema tutengeneza aina yetu ya muziki’’

swahiliInfo.blog pia imepata nafasi ya kujua sahabu hasa ya kubadilisha  aina ya muziki wake kutoka kwenye kurap juu ya beat za HipHop na Crank na kuanza kurap kwenye beat flan za kuchezeka zaidi kama afro Pop wengine huzita za kibongo flava

‘’Mimi ni muafrika na Afrika asili yetu ni ngoma ngoma basi kama narap narap kwenye mdundo mwenye asili ya kiafrika ,yani nimeamua ku-change muziki kwa sababu kubwa kupanua wigo wangu ,pili naweza nikasema ni muziki nilio ona unaweza ukanitambulisha  na kunitoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine akajulikana huyu anatoka tanzania’’ 
Msikilize hapa...

0 comments: