Star wa "Prison Break", Wentworth Miller a.k.a Michael Scofield,
amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga), katika barua ya wazi
aliyoiandika kwenda kwa Directoe wa St. Petersburg International Film Festival (tamasha la filamu la kimataifa la St. Petersburg)
Muigizaji
huyo (41) ameandika barua hiyo kukataa mualiko uliokuwa ukimtaka
kuhudhuria tamasha hilo linalofanyika nchini kwao Russia na kwa mara ya
kwanza kupitia barua hiyo amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga).
"Asante
kwa ukarimu wa mualiko wako, nikiwa kama mtu ambaye amefurahia
kutembelea Russia kwa miaka ya nyuma na naweza pia kudai shahada ya
asili ya kirusi, ningefurahi kusema ndio, hata hivyo nikiwa kama shoga
lazima nikatae". amesema Miller
Miller akaendelea kusema ... nasumbuliwa sana na tabia ya sasa dhidi ya na jinsi wanavyochukuliwa mashoga na wanawake na serikali ya Urusi.
"hali hii haikubaliki kabisa, na mimi siwezi kwa dhamira nzuri kushiriki katika tukio la kusherehekea linaloandaliwa (wenyeji) na nchi ambayo watu kama mimi kwa mfumo uliopo wananyimwa haki zao za msingi za kuishi na kupenda kwa uwazi"
akamalizia kwa kusema.. kama hali hii itarekebishwa, nitakuwa huru kufanya uchaguzi tofauti.
0 comments:
Post a Comment