Monday, May 12, 2014

Donald Sterling aomba radhi kwa ubaguzi wa rangi, anaamini alitegwa na mpenzi wake 'nilitegwa kuingia kwenye kosa kubwa'

Donald Sterling aomba radhi kwa ubaguzi wa rangi, anaamini alitegwa na mpenzi wake
Mmiliki wa Clippers, Donald Sterling ameomba radhi kwa kosa alilofanya la kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu weusi wakati akiongea na mpenzi wake kwa njia ya simu wiki kadhaa zilizopita na maneno yake kurekodiwa na kusambazwa.

 
Donald Sterling ambaye amefungiwa kujihusisha na mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani ameomba radhi wakati akifanya mahojiano mtangazaji wa CNN, Anderson Cooper.
“I'm a good member who made a mistake and I'm apologizing and I'm asking for forgiveness. Am I entitled to one mistake, am I after 35 years? I mean, I love my league, I love my partners. Am I entitled to one mistake? It's a terrible mistake, and I'll never do it again.”
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 amekiri kuwa aliyasema yote hayo, lakini amesema alipokuwa anayasikiliza maneno yake alishindwa kuelewa ni kwa nini alisema yote hayo na kwa nini mrembo wake mwenye umri wa miaka 20 alimfanya aseme vile.
“Ninapoisikiliza ile tape, sifahamu ni jinsi gani naweza kusema maneno kama hayo…sifahamu kwa nini yule msichana alinifanya niseme mambo yote yale.” Alisema Mzee Sterling.
Mtangazaji huyo alimuuliza kama anafikiri kwamba aliwekewa mtego wa makusudi ili afunguke vile.
“Ni kweli, nilitegwa. Namaanisha kuwa hivyo sivyo ninavyoongea. Daima siongei kuhusu watu kwa kitu kimoja. Huwa naongea kuhusu ideas na mambo mengine. Sizungumzi kuhusu watu.”
Mmiliki huyo wa Clippers, aliwashitua wengi baada ya maongezi yake na mpenzi wake yenye dakika 10 kuwekwa TMZ na kuwasha moto ambao ulipelekea kufungiwa maisha kujihusisha na mpira wa kikapu katika ligi ya Marekani ‘NBA’ na kulipishwa faini ya $2.5 million.
Watu mbalimbali akiwemo Commissioner wa NBA, Adam Silver wameendelea kumshinikiza ili aiuze Clippers.
Credit:times fm

0 comments: