Saturday, May 10, 2014

Mabadiliko: The Jump Off ya Times Fm kucheza asilimia 90 nyimbo za wasanii wa Tanzania siku zote

Mabadiliko: The Jump Off ya Times Fm kucheza asilimia 90 nyimbo za wasanii wa Tanzania siku zote

Kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm kimefanya mabadiliko katika upigaji wa muziki wake ambapo kimeamua kujikita zaidi katika muziki wa Tanzania kwa asilimia 90 na asilimia 10 tu zitasikika nyimbo za nje ya Tanzania. 

 

Mtangazaji wa The Jump Off Jabir Saleh ameeleza sababu za kufanya mabadiliko hayo kuwa inatokana na utafiti walioufanya kama timu na kuzingatia maoni na malalamiko ya wasanii wa nyumbani Tanzania kuhusu nafasi wanayopata kwenye media.
“Tumeweza kufanya utafiti mbalimbali na kuongea na wasanii kwa mfano Izzo Bizness, lakini pia kupitia segment ya ‘Straight From The Street’ na tumeona kwamba wanamuziki wa nyumbani wanalalamika kuwa hawapati support ya kutosha kulinganisha na wasanii wa  nje kama Nigeria na marekani, ukizingatia kuwa katika nchi hizo hawatoi sapoti ya kutosha kwa muziki wetu.” Amesema Jabir Saleh.
“Lakini pia ni kumpa nafasi msikilizaji aweze kusikiliza zaidi muziki wa nyumbani ambao umekuwa ukizingumzia maisha ya hapa hapa kwetu. Kwa hiyo hii ni nafasi kwa wasanii kuweza kujisogeza zaidi katika kipindi cha The Jump Off, lakini pia ni kutaka kupromote zaidi muziki wetu ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa Times Fm inasikika pia kwa njia ya mtandao.”
Hata hivyo, Jabir amesema segments zote za kipindi hicho zinaendelea kama kawaida.  
The Jump Off ya 100.5 Times Fm inakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili kamili hadi saa nne kamili usiku.
Unaweza kusikiliza online kupitia tovuti ya Times fm, kisha bofya sehemu iliyoandikwa "Listen"

0 comments: