Rapper Frech Montana (29 )huenda akamvisha pete ya uchumba mpenzi wake Khloe kardashian hivi karibuni.
Khloe ambaye aliachana na mumewe Lamar
Odom December mwaka jana walieishi pamoja kwa miaka minne kwa madai alikuwa
akimsaliti na pia ni mtumiaji wa madawa ya kulevya inasemekana amekuwa
akishinikiza talaka yake ikamilike mapema iwezekanavyo.
Chanzo cha karibu cha wawili hao
kimeliambia jarida la Life & Style Weekly kuwa Frech ameanza kufikiria
kuhusu pete ya uchumba na wamekuwa wakizungumzia malengo yao ya mbeleni na
huenda wakafunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.
Mahusiano ya Fresh na Khloe yamekuwa
kwa haraka na hivi karibuni Khloe
alimsadia kutafuta nyumba Montana mitaa ya Los Angeles ili wawe karibu..
0 comments:
Post a Comment