Thursday, July 31, 2014

Iyanya atoa ushauri kwa Wizkid na Davido kuhusu beef kati yao

Iyanya atoa ushauri kwa Wizkid na Davido kuhusu beef kati yao
Taarifa za kuwepo beef kati ya wasanii wakubwa wa Nigeria Wizkid na Davido wakitambiana nani anafunika zaidi zinaendelea kukorezwa na tweets za vijembe kati yao kila kukicha.

Ingawa wawili hao waliwahi kuonekana katika picha ya pamoja na kutoa ishara ya kumaliza tofauti zao, bado maandishi yao yanaonekana kuwa mwiba kwa kila mmoja.
Mkali wa Kukere ameamua kutoa ushauri wake kwa wasanii wa Nigeria, ushauri ambao unaonekana kumwagusa moja kwa moja Wizkid na Davido ingawa hakuwataja majina.
“Acheni kuongea!!! Tuachie muziki zaidi!!! Tuwaburudishe mashabiki!!! Acheni chuki!!! Maombi yangu ni kwamba wote tufanikishe.”

0 comments: