Saturday, June 07, 2014

Diamond kurekodi wimbo na Mafikizolo


Leo ni siku ambayo mashabiki wa muziki Afrika na duniani wataiangalia Durban kwa macho mawili au kusikiliza kinachoendelea huko kwa masikio yote kwa kuwa MTV MAMA zitatolewa usiku.


Diamond Platinumz ambaye ni mwakilishi wa Tanzania pekee anaeshindania tuzo hizo, anazidi kuongeza connections na kujitanua zaidi wakati akisubiria utoaji wa tuzo hizo.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana kwa ajili ya MTV MAMA , kundi la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini lilithibitisha kuwa linafanya mazungumzo nae kuhusu kushirikishana kwenye wimbo.
Diamond anawania tuzo katika vipengele viwili. Msanii bora wa kiume, na wimbo bora wa kushirikishana (Number One Remix aliofanya na Davido).

0 comments: