Kuni la muziki kutoka Marekani Cali Swag District limempoteza memba wa kundi
hilo JayAre ambaye amefariki jana ijumaa ,
Kwa mujibu wa MTV News Cheron Childs AkA JayAre amefariki kutokana na kusumbuliwa
na sickle cell anemia ambapo siku ya
alhamisi alikimbizwa hospital lakini madaktari walishindwa kuokoa uhai wake.
Rafiki yake wa karibu ambaye walikuwa katika kundi moja la Cali Swag
District (CSD) Smoove Da General alitweet kuhusu kifo cha Msanii huyo
“Sickle cell took my brother away
from me today…with that being said I’m proud to know that with that disease he
made the best of his life,”
“Rest in peace Jayare I’m gonna miss u forever ..I will never get over
this..but I know God got u..and I know You got me.”
Kundi hilo lilianza likiwa na wasanii wanne hivi sasa limebakia na wasanii
wawili kwani JayAre sio msanii wa kwanza
wa kundi la Cali Swag District kupoteza
maisha akiwa na umri mdogo , May 2011, Montae “M-Bone” Talbert msanii mwingine
kutoka katika kundi hilo alifariki dunia kwa kupigwa risasi.
Kundi hili la Cali Swag District lilipata umaarufu mwaka 2010 kupitia wimbo wao
uliuza platinum “Teach Me How to Dougie” wimbo ulikuepo kwenye albam yao ya
kwanza The Kickback. Mwanzoni mwa mwaka huu walitoa Mixtape The
District wakiwa wamewashirikisha Nipsey Hussle, Ty Dolla $ign, na Waka
Flocka Flame.
0 comments:
Post a Comment