Wakati nchi nyingi hivi sasa zimelegeza sheria ya matumizi ya marujuana ,Jamaica pia inampango wa kubadilisha sheria za matumizi ya bangi ambayo hutambulika kama ni dawa za kulevya.
kwa mujibu wa TIME,waziri wa sheria nchini humo Mark Golding alitangaza mabadiliko hayo siku ya jumanne wiki hii kuwa sheria hiyo itaaanza kutumika bbaada ya msimu wa joto kumalizika.
Waziri huyo amesema bunge limeridhia kufanya mabadiliko kwenye sheria kuhusu ganja ambapo sheria hiyo itahusisha watumiaji wa kawaida ,uvutaji wa bangi sehemu isiyo hadharani na pia itawahusu wanao vuta kwa ajili ya matibabu ya kiafya
Sheria hiyo ikibadilishwa itawawezesha watumiaji wa bangi kulipa faini ndogo na kufanya kazi za kijamii badala ya kwenda jela.
Kwa mujibu wa waziri huyo moja kati ya sababu ya zilizo fanya kulegeza sheria hiyo ni kutokana na vijana wengi kujikuna na rekodi ya kuvunja sheria baada ya kukamatwa na makosa ya kuvuta bangi kitu ambacho kinawafanya wakose sifa za kufanya vitu vingine kama kupata kazi na kupata visa kwa ajili ya kusafiri
0 comments:
Post a Comment