Tuesday, June 03, 2014

Mkurugenzi wa Instagram asema ni marufuku kuweka picha za Utupu hata kama ni mtu maaarufu.

https://lh3.ggpht.com/vFpQP39LB60dli3n-rJnVvTM07dsvIzxrCL5xMiy1V4GV4unC1ifXkUExQ4N-DBCKwI=w300

Muasisi wa mtandao wa kijamii wa istagram ameiambia tovuti ya bbc newbeat kuwa sheria za mtandao huo kuhusiana na kuonesha sehemu za siri zina “usawa” akimaanisha hazichagui mtu maarufu au mtu wa kawaida.

Instagram imekumbana na shutuma kali baada ya kuondoa picha zinazoonesha sehemu za chuchu za wanawake.
Mkurugenzi wa instagram Kevin Systrom amesema sheria za kampuni yake zinalenga kufanya  mtandao huo wa kijamii kuwa salama kwa watoto na wakubwa.

Kauli hiyo imekuja baada ya scout willis mtoto wa kike wa mcheza filamu maarufu wa Hollywood Bruce Willis ,kupinga moja ya picha yake kuondolewa insagram .
Rihana ambaye alikuwa na marafiki ,illion 1.3 kwenye Instagram kabla ya kuufunga ukurasa wake ,alitweet kuunga mkono kampeni hiyo ..

0 comments: