Tanzania
ni miongoni mwa nchi tano za bara la Africa zilizochaguliwa na rapper Sean
Carter aka Jay-Z kwaajili ya kutumbuiza kama sehemu ya ziara yake ya wiki saba
ya dunia. Ziara hiyo ni kwaajili ya kutangaza uelewa kuhusu tatizo la maji
duniani. Inatarajiwa kuanza September 9 nchini Poland na kuzunguka mabara ya
Ulaya, Africa, Asia na kumalizia Australia.
Barani
Africa ataanza na show jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee
October 4 kisha Accra, Ghana, Lagos, Nigeria, Luanda, Angola, Cape Town,
Durban, na Johannesburg, Afrika Kusini
Source: okayafrica.com
0 comments:
Post a Comment