Siku chache baada ya Rapper Jay Z kufungua kampuni ya uwakala wa
wanamichezo Roc Nation sports, taarifa zilizoendea kwenye mitandao ni kwamba
rapper huyo anajipanga kumsaini mshambuliaji wa Brazil Neymar kwenye kampuni hiyo
.
“Roc Nation” iinataka kujikita katika michezo yote hasa
soka, ikijaribu kuwafanya wachezaji kuwa mastaa wa kweli duniani kwa kuwa na
mikataba minono na makampuni tofauti. Ndio maana Neymar kwa sasa amepewa
kipaumbele kuwa mcheza soka wa kwanza kusainiwa kwenye kampuni ya Jay Z."
Neymar ataungana na Robinson Cano wa New York Yankees na
Skylar Diggins wa WNBA katika listi ya wanamichezo waliopo katika kampuni ya ya
Jigga inayoanza kukua kwa kasi japo imeanzishwa mapema mwaka huu.
Lakini Jay Z atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa kampuni ya masoko ya michezo inayomilikiwa na gwiji wa Brazil Ronaldo, ambayo ilimsaini Neymar kumwakilisha katika haki zake za taswira yake mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment