Tuesday, July 15, 2014

Fresh Montana akaribia kumvisha Khloe Kardashian.
Rapper Frech Montana (29 )huenda akamvisha pete ya uchumba mpenzi wake Khloe kardashian hivi karibuni.
Khloe ambaye aliachana na mumewe Lamar Odom December mwaka jana walieishi pamoja kwa miaka minne kwa madai alikuwa akimsaliti na pia ni mtumiaji wa madawa ya kulevya inasemekana amekuwa akishinikiza talaka yake ikamilike mapema iwezekanavyo.

Chanzo cha karibu cha wawili hao kimeliambia jarida la Life & Style Weekly kuwa Frech ameanza kufikiria kuhusu pete ya uchumba na wamekuwa wakizungumzia malengo yao ya mbeleni na huenda wakafunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.

Mahusiano ya Fresh na Khloe yamekuwa kwa haraka na hivi karibuni Khloe  alimsadia kutafuta nyumba Montana mitaa ya Los Angeles ili wawe karibu..

0 comments: