Thursday, May 29, 2014

Mosey Radio matatani kwa kupanda marujuana nyumbani kwake..

0 comments
Mwanamuziki kutoka Uganda  Mozey Radio ameingia matatani baada ya kukamatwa kwa makosa mawili ikiwemo kupigana hadharani na pia kupanda bangi nyumbani kwake.

Nuh Mziwanda asimulia alivyokutana na Shilole

0 comments
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/03/Nuhu-Mziwanda-akiwa-na-Shilole.jpg
Hakuna asie fahamu kama Nuh Mziwanda na shilole ni wapenzi ,sasa Nuh akifanya mahojiano na kipindi cha Trending Africa cha 100.5 times fm amezungumzia jinsi alivyo kutana na shilole aka shishi mpaka wakawa wapenzi.

Tuesday, May 27, 2014

Yemi Alade kutoa albam "King of queens"

0 comments
 Yemi Alade
Baada ya wimbo wa Johnny kufanya vizuri barani Africa muimbaji wa wimbo huo Yemi Alade anatarajia kutoa albam yake ya kwanza.

MAYWEATHER AMUOMBA RADHI MKE WA T.I NA WANAE KWA UGOMVI KATI YAKE NA T.I NA KUMUITA ‘KAHABA’

0 comments

 
Bondia Floyd Mayweather amemuomba radhi mke wa T.I, Tiny kufuatia ugomvi kati yake na T.I ambao ulipelekea yeye kumtaja kwa jina la kumdhalilisha ‘kahaha’.

Tuesday, May 20, 2014

Ciara ajifungua mtoto wa kiume

0 comments


  photo ScreenShot2014-05-20at24513PM_zps53d719a4.png
 Pongezi kwa wanamuziki Ciara na  Future ambao wamepata mtoto wa kiume jumatatu wiki hii .
Mtoto huyo amekuwa wa kwanza kwa Ciara mwenye umri wa miaka 20 na anakuwa mtot wan ne kwa Future ambaye tayari anawatoto watatu aliowapata hapo mwanzo.

Ray J kumpa Kim K zawadi ya ndoa sehemu ya mauzo ya mkanda wao ngono..

0 comments
 
Ray J amepanga kuwapa  Kim Kardashian na Kanye West zawadi ya  dola laki 47 kama zawadi ya ndoa yao pesa ambayo amedai inatokana na mauzo ya mkanda wa ngono waliotengeneza miaka iliyopita.

50 cent akasirishwa na kuto kualikwa katika mahafali ya mwanae akimaliza high school.

0 comments
Kufuatia kuenea kwa habari za 50 kuto kuhudhuria mahafali ya mwanae wa kwanza wa kiume Marquise akimaliza high school mwinyoni mwa wiki na kupelekea watu kumsema vibaya jamaa amelazimika kutolea ufafanuzi swala hilo ambapo kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilicho zungumza na TMZ kimesema 50 hakufika katika mahafali hayo kutokana na kuto kualikwa wala kujua wapi yalikuwa yakifanyika

Monday, May 19, 2014

Cyrill asema ugumu wa taratibu za kutunza Camera za kuazima nje ya nchi ni kikwazo, kushuti 'Alowa' na director wa Kenya

0 comments

Cyrill asema ugumu wa taratibu za kutunza Camera za kuazima nje ya nchi ni kikwazo, kushuti


Ubora wa video ni moja kati ya hatua kubwa wanayoifanyia kazi wasanii wengi wa Tanzania ili video hizo zinapoifunika audio nzuri wanazofanya zikubalike katika vituo vikubwa vya runinga vya kimataifa.
Wapo wasanii kadhaa ambao kwa kutumia waongozaji wa Tanzania video zao zimeweza kuchezwa MTV na Channel O.

Muziki,pesa &ndoa: Mambo 10 usiyo yajua kumuhusu Wizkid

0 comments
Wizkid
1. Wizkid ngoma zake zote huandika mwenyewe
2. Wizkid hana mpango wa kuoa.
3.  vitu vitatu anavyo vipenda wizkid katika nchi ya afrika kusini kwanza watu wa south afrika ,pili muonekano wa mazingira ya south afrika tatu wanawake
4. Wizkid aina ya viatu anavyo penda ni  Jordans
5. na ana pair 122 za viatu
6. Wizkid ana tattoo 11 zikiwepo  tattoo za jina la mama yake na mwanae
7. Wizkid baba yake alishawahi kuwa mwanasiasa
8. Wizkid huwa hatizami mpira wa miguu

9. Wizkid huwa hatizami mpira wa miguu
10.Watu wanao mshawishi kufanya mziki ni Fela kuti na  Asa

Lupita Nyong'o anatarajia kucheza kama mfanyakazi wa ndani kwenye movie mpya ' Southpaw’

0 comments
lupita
Mshindi wa tuzo za Oscar Muigizaaji wa kike kutoka nchini kenya Lupita Nyong'o ambaye amjipatia umaharufu mkubwa kupitia filamu ya '12 years a slave' anatarajia kuendeleza makali yake katika filamu mpya inaitwa  ' Southpaw’.

Thursday, May 15, 2014

MWIMBAJI WA MUZIKI WA DANSI AMINA NGALUMA AFARIKI DUNIA

0 comments

MWIMBAJI nyota wa zamani wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound, African Revolution 'Wana Tamtam', Amina Ngaluma 'Japanese' amefariki dunia akiwa nchini Thailand baada ya kupatwa na uvimbe kichwani. Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors. Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam.  
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!…

SAUTI:Makamua kulipwa pesa baada ya wimbo wake kuchezwa kwenye Radio za Sweden..

0 comments
 
Makamua amesema wimbo alio mshirikisha Saraha Don’t cry unafanya vizuri nchini Sweden na huenda hivi karibuni akaanza kupokea malipo kutokana na wimbo huo kuchezwa kwenye vituo vya radio nchini humo.

Tazama video ya diamond akizungumzia kuchaguliwa kuwania tuzo za BET.

0 comments

Credit :Jestina George

Jay Z kuwa Best Man wa Kanye West kwenye ndoa yake na Kim Kardashian .

0 comments

Jay Z To Act As Best Man In Kanye West & Kim Kardashian Wedding 
kwa mjibu wa mtandao wa  Radar Online  , Jay Z anajipanga kuwa msimamizi wa kanye west kwenye ndoa yake na Kim K iliopamgwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu Paris Ufaransa.

Video ya Jay Z akishambuliwa na Solange kwenye lift ilinunuliwa na TMZ kwa shilingi million 400! Aliyeivujisha atimuliwa kazi"

0 comments
jay z_beyonce_solangeThe Standard Hotel lilipotokea tukio la dada wa Beyonce, Solange Knowles kumpiga Jay Z kwenye lift imembaini mfanyakazi aliyevujisha CCTV video ya tukio hilo,
lililotokea May 5 na kumchukulia hatua ya kumtimua kazi kwa kukiuka sera ya usalama wa hotel hiyo.

Wednesday, May 14, 2014

Soma alichokiandika diamond baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo za BET..

0 comments

Baada ya kutajwa kuwania tuzo za BET za marekani mwaka 2014 kupitia kipengele cha best international act:Africa, Diamond amewatumia ujumbe mashabiki wake kupitia Twitter wa  kuwashukuru huku pia akiwataka kumpigia kura ili aweze kushinda tuzo hizo..

Diamond Platnumz atajwa kuwania tuzo za Bet 2014

0 comments
Diamond (2)

Baada ya kunyakua tuzo 7 za KTMA 2014, na kuwa nominated katika tuzo za MTV ‘MAMA’ nchini Afrika Kusini, sasa Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo kubwa zaidi za kimataifa BET Awards za nchini Marekani.

Tuesday, May 13, 2014

wasanii wazungumzia sakata la Jay Z na Solange

0 comments
 
baada ya kuvuja kwa video inaonesha Jay Z akipigwa na mdogo wake Beyonce, Solage wakiwa ndani ya lift baadhi ya wasanii wametoa maoni yao juu ya sakata hilo ambalo limechukuua Headline karibia kila chombo cha habari..

Video: Mdogo wake Beyonce ampiga Jay Z ndani ya Lift

0 comments
Video: Mdogo wake Beyonce ampiga Jay Z ndani ya Lift
Jay Z alijikuta akishambuliwa na mdogo wake Beyonce anaejulikana kwa jina la Solange wakati wakiwa ndani ya lift.
Beyonce, Jay Z na Solange walikuwa wakitoka kwenye After Party huko New York iliyofanyika Standard Hotel. Solange alimshambulia Jay Z kwa Mateke na makofi huku Beyonce akiwa amesimama anaangalia wakati Jigga akijaribu kujilinda.
Sababu ya Solange kufanya tukio hilo bado haijafahamika.

Monday, May 12, 2014

Obama ampongeza mchezaji wa American Football aliejitangaza hadharani kuwa na tabia za ushoga

0 comments
Obama ampongeza mchezaji wa American Football aliejitangaza hadharani kuwa na tabia za ushoga
Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya American Football (National Footbal League), Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza wa mpira wa miguu kutangaza kuwa anajihusisha na tabia za ushoga.
Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini marekani.

Hermy B aandika barua ya wazi inayoeleza kwa kina yaliyotokea B'Hitz na mpango wao mpya, 'It's a new Chapter'

0 comments

Hermy B aandika barua ya wazi inayoeleza kwa kina yaliyotokea B 
 Producer na CEO wa Bhitz Music Group, Hermy B ameandika barua ya wazi akielezea yaliyowahi kutokea Bhitz, uamuzi na mpango wao mpya.

Donald Sterling aomba radhi kwa ubaguzi wa rangi, anaamini alitegwa na mpenzi wake 'nilitegwa kuingia kwenye kosa kubwa'

0 comments
Donald Sterling aomba radhi kwa ubaguzi wa rangi, anaamini alitegwa na mpenzi wake
Mmiliki wa Clippers, Donald Sterling ameomba radhi kwa kosa alilofanya la kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu weusi wakati akiongea na mpenzi wake kwa njia ya simu wiki kadhaa zilizopita na maneno yake kurekodiwa na kusambazwa.

Saturday, May 10, 2014

Mabadiliko: The Jump Off ya Times Fm kucheza asilimia 90 nyimbo za wasanii wa Tanzania siku zote

0 comments
Mabadiliko: The Jump Off ya Times Fm kucheza asilimia 90 nyimbo za wasanii wa Tanzania siku zote

Kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm kimefanya mabadiliko katika upigaji wa muziki wake ambapo kimeamua kujikita zaidi katika muziki wa Tanzania kwa asilimia 90 na asilimia 10 tu zitasikika nyimbo za nje ya Tanzania. 

Rais Kikwete afanya mazunguzo na Samatta na Ulimwengu nchini Congo..

0 comments
 

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo amewatembelea washambuliaji wawili Watanzania wanaocheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emannuel Ulimwengu.

Thursday, May 08, 2014

Michelle Obama, Drake, Angelina Jolie wajiunga kwenye kampeni ya #BringBackOurGirls

0 comments

 Michelle Obama
Mke wa rais wa marekani Michalle Obama amejiunga na Watu maarufu duniani  katika kampeni ya #BringBackOurGirls  kushinikiza kuachiwa kwa wasichana ambao ni wanafunzi  zaidi ya 200 walitekwa  nchini Nigeria na kikundi cha Boko Haram tangu April 14, 2014. 

VIDEO :Rapper Scarface amesema haoni sababu ya Donald Sterling kuomba msamaa baada ya kitendo chake ubaguzi ..

0 comments

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/0/02/Scarface_(rapper).jpg
Baada ya chama cha mpira wa kikapu nchini marekani NBA kumfungia maisha mmiliki wa timu ya kikapu L.A clippers Donald Sterling ,baada ya kupatikana na hatia ya ubaguzi kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na mpenzi wake V. Stiviano akimwambia hataki kuona akipeka watu weusi katika michezo yake ,kufuatia kitendo hicho watu wengi wamekuwa wakimtaka Sterlin aombe msamaa lakini imekuwa kinyume kwa rapper Scarface .

Wednesday, May 07, 2014

MFAHAMU MWANAMKE WA KWANZA KUWA KOCHA WA KLABU YA LIGI KUBWA ULAYA.

0 comments

KLABU ya Daraja la Pili Ufaransa, Clermont Foot imemuajiri mwanamama Helena Costa kuwa mocha wao mpya.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 39 atakuwa mocha wa kwanza wa kike kuongoza timu ya maharaja mawili ya juu katika Ligi za Ulaya.
Costa kwa sass ni mocha wa timu ya taiga ya wan awake ya Iran ambaye awali alifundisha timu za wan awake za Qatar na Benfica. Pia amewahi kufanya kazi na mabingwa wa Scotland, Celtic.
Mwanamama kazini: Helena Costa (kulia) ndiye mocha mpya wa Clermont Foot ya Daraja la Pili Ufaransa

Audio: Profesa Jay asema wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri hawawaheshimu wasanii wakongwe

0 comments
 Audio: Profesa Jay asema wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri hawawaheshimu wasanii wakongwe
Profesa Jay ni moja kati ya wasanii walioleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya na kuwashawishi watu wengi waupende na kuusikiliza mwishoni mwa karne ya 20.

Rapper Rich Hommie adondoka kwa kifafa..

0 comments
Rapper Rich Homie Quan Hospitalized After Suffering Twin Seizures
Rapper Rich Homie Quan  jana jumanne jioni alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kupata kifafa (seizures) na kudondoka wakati akifanya video huko Atlanta.

Jay Jay Okocha amesaini mkataba wa kuwa balozi wa kinywaji cha Bullet Energy ..

0 comments

Jay Jay Okocha  


Mwanasoka mkongwe  Austin ‘Jay Jay’ Okocha amesaini mkataba wa kuwa balozi wa kinywaji cha  Bullet Energy ,mchezaji huyo wa zamani wa   Bolton Wanderers FC ameungana na muigizaji wa kike  Chika Ike katika dili hilo ambaye sura yake imekuwa kitumika kukitangaza kinywaji hicho .

Tuesday, May 06, 2014

VIDEO:Tyrese aponda reality Tv shows asema zinachangia kuharibu mahusiano..

0 comments

Tyrese amesema blogs ,vyombo vya habari na reality TV vinaharibu mahusiano ya wapenzi wengi kwa kuwa vimeegemea kwenye upande wa mabaya  na kutalakiana kuliko kumulika mazuri katika mahusiano ya ndoa.

Thursday, May 01, 2014

BAADA YA DOMAYO NA KAVUMBANGU KUSAJILIWA NA AZAM FC ,YANGA YATOA TAMKO..

0 comments
Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.