Tuesday, May 06, 2014

VIDEO:Tyrese aponda reality Tv shows asema zinachangia kuharibu mahusiano..


Tyrese amesema blogs ,vyombo vya habari na reality TV vinaharibu mahusiano ya wapenzi wengi kwa kuwa vimeegemea kwenye upande wa mabaya  na kutalakiana kuliko kumulika mazuri katika mahusiano ya ndoa.


Tyrese ametumia dakika nne kujirecord kipande cha video kwa ajili ya mashabiki wake kuzungumzia mtizamo wake juu swala hili ambapo amsema kutokana na kile kinachofanyika na vyombo vya habari hivi sasa kama ,blogs,website ,majarida na vipindi vinavyo zungumzia maisha halisi anaamini ni mtindo mpya wa shetani kufanya kazi yake.

“Vyombo vya habari vinakazi ya kufanya , na vinafanya, lakini kwasasa watu waliopo kwenye mahusiano mazuri hawawezi kutokea kwenye majarida pendwa ni mpaka watangaze kutengana na kufanya talaka kuwa maarufu kuzidi kilichofanyika ndani ya ndoa’’..
Tyrese ametoa wito kwa waandaaji wa vipindi vya maisha halisi (reality shows) na majarida kumulika vitu vizuri vinavyotokea katika mahusiano,familia nandoa  kuliko kuzingazitia mabaya na vitu vilivyo shindwa kufanyika..
“Sasa hivi kinachotokea nyumbani kwako ni kile  unachoangalia kwenye kipindi  kama ‘The Housewives’ au chochote kinacho onesha maisha halisi (reality tv) Unagombana nyumbani kwako, kwenye ndoa yako na familia yako na moja kwa moja unagundua vyote vinasababiswa na vitu mnavyoviona kwenye TV”
Ameendelea kusema mwanamke anakaa anaangalia TV analinganisha matatizo ya nyumbani kwako na ugomvi anao uona kwenye TV na yule mwanamke alie lalamika anakuwa shahidi yake wakati yale sio mahusiano yake na hayahusiani na matatizo yake ,huku nikutengeneza matatizo katika familia amesema Tyrese.
Tyrese amewasi wale walio na furaha ndani ya mahusiano kuendelee kuwa hivyo bila kujali kinachoendelea duniani,bila kukubali kuishi maisha yasio yao.

0 comments: