Thursday, May 08, 2014

VIDEO :Rapper Scarface amesema haoni sababu ya Donald Sterling kuomba msamaa baada ya kitendo chake ubaguzi ..


http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/0/02/Scarface_(rapper).jpg
Baada ya chama cha mpira wa kikapu nchini marekani NBA kumfungia maisha mmiliki wa timu ya kikapu L.A clippers Donald Sterling ,baada ya kupatikana na hatia ya ubaguzi kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na mpenzi wake V. Stiviano akimwambia hataki kuona akipeka watu weusi katika michezo yake ,kufuatia kitendo hicho watu wengi wamekuwa wakimtaka Sterlin aombe msamaa lakini imekuwa kinyume kwa rapper Scarface .


Rapper huyo kutoka Houston amesema  Sterling hatakiwi kuomba msamaa kutokana na alicho kisema ,na akahoji ni kipi hasa sterling alichokifanya anatakiwa kuomba msamaa

“si hisi kama anatatakiwa kuomba msamaa ,kwanini afanye hivyo kwa kipi ? aombe msamaa kwasababu hapendi watu weusi ?kwanini uombe msamaa kwa kitu kama hicho "amesema Scarface

Scarface pia akakosoa utofauti wa umri kati ya   Sterling na mpenzi wake V. Stiviano.ambapo amesema V.Stiviano ni mtoto mdogo wa Sterling ambaye anamiaka 80.

“upo ndani ya mapenzi na mtoto wake ambaye ni kama mjukuu wako ,una miaka  80 unawezaje kuwa kwenye mapenzi na mtu ambye ni sawa na mtoto wako lakini kusema haitaji watu weusi kwenye michezo yake siwezi kumlaumu na ni kwa watu wote wenye mtazamo kama huo ,kama mtu hakupendi kutokana na rangi ya ngozi yako ni tatizo lake  man mimi napenda jinsi nilivyo ,kwa mtu anae kuchukia jinsi ulivyo ni wazi anapenda kuwa kama wewe' amesema Scarface

 
Scarface amekuwa na mtizamo tofauti na wasanii wengine kama Snoop Dogg ,Meek MILL NA Lil Wyne ambao waliojitokeza kuzungumzia ishu hiyo ya Donald Sterling,
kwa upande wa Lil wyne alisema .“kama ningekuwa shabiki wa Clipper , nisingeendelea kushabika timu hiyo ,lakini kaka ningekuwa nachezea Clipper usingeniona uwanja tena nimelia jezi ya timu hiyo"'

0 comments: