Thursday, May 15, 2014

Video ya Jay Z akishambuliwa na Solange kwenye lift ilinunuliwa na TMZ kwa shilingi million 400! Aliyeivujisha atimuliwa kazi"

jay z_beyonce_solangeThe Standard Hotel lilipotokea tukio la dada wa Beyonce, Solange Knowles kumpiga Jay Z kwenye lift imembaini mfanyakazi aliyevujisha CCTV video ya tukio hilo,
lililotokea May 5 na kumchukulia hatua ya kumtimua kazi kwa kukiuka sera ya usalama wa hotel hiyo.

May 12, TMZ ilipost video ya dakika tatu iliyomuonesha Solange akimshambulia shemeji yake Jigga huku akizuiwa na mlinzi na Beyonce akiwa pembeni akitazama kinachoendelea.
Baada ya video hiyo kusambaa uongozi wa hotel hiyo ulisema unachunguza swala hilo.
Kwa mujibu wa Page Six, inasemekana video hiyo iliuzwa kwa TMZ kwa $250,000 ambazo ni ni sawa na milion mia 400 za kibongo pesa ambazo hivi sasa
zimemtokea puani mfanyakazi huyo kwa kupoteza kibarua chake.


0 comments: