Wednesday, May 07, 2014

Audio: Profesa Jay asema wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri hawawaheshimu wasanii wakongwe

 Audio: Profesa Jay asema wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri hawawaheshimu wasanii wakongwe
Profesa Jay ni moja kati ya wasanii walioleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya na kuwashawishi watu wengi waupende na kuusikiliza mwishoni mwa karne ya 20.

 
Wapo wasani wengi wapya na wanaofanya vizuri ambao wanaeleza wazi kuwa walianza muziki wakiwa shuleni baada ya kusikiliza albam kama ‘Kubwa Kuliko’ ya HBC au solo albam ya Profesa Jay ‘Machozi Jasho na Damu’.
Q Chilla ni mmoja kati ya wasanii wakubwa ambao wanaeleza wazi kuwa walivutiwa kwenye game na Profesa Jay na kufanya vizuri pia hadi wakashirikiana kwenye wimbo ‘Msinitenge’.
Ukongwe wake kwenye game na muendelezo wa kuwa na stamina kwenye game kwa kipindi chote vinamfanya aonekane kwenye list ya nyimbo mpya kali zinazofanya vizuri, na mwaka huu ameachia ‘Kipi Sijasikia’ akiwa amemshirikisha Diamond ambaye ni miongoni mwa wasanii wapya wanaofanya vizuri sana Tanzania na nje ya nchi.
Tovuti ya Times Fm ilipiga story na Profesa Jay kutaka kujua kama anaona anapewa heshima ya kutosha na wasani wapya ambao wanafanya vizuri kwa kipindi hiki.
“Wengi wakiwa na mimi wanafanya hivyo lakini wengi wanadisrespect. Na mimi siku moja nilisikitika sana nilipoenda kwenye kumbi moja ya starehe nikamkuta mmoja kati ya malegend amewekwa pembeni halafu hawa watoto wa juzi tu ambayo yeye ndiye amewatengenezea barabara wanayopita wanapita watatu wanne watano halafu yeye amezuiwa kwa sababu hawamfahamu.” Amesema Profesa.
“Watoto wengi wa sasa hivi hawawajui malegend waliopita nyuma kwa sababu nadhani wakati tunafanya muziki hiyo miaka ya 95 ndio walikuwa ndio wanazaliwa, wengine hawajaja down town, wengine hawajui hata kama wanaweza kufanya muziki. Na mimi nimewakuta hao malegend ambao niliwakuta wamewekwa pembeni watu wakiingia hawa watoto wa sasa hivi.” Ameongeza.
Ameeleza kuwa lazima wasanii wote wawaheshimu wakongwe ambao waliweka nguvu pia katika muziki wao kama ilivyo Marekani ambapo wakongwe kama KRS One wanaendelea kuheshimiwa na kupewa nafasi.
“Ni juzi tu tumeanza huu muziki lakini watu wanashindwa kutoa respect. Watu wanapotoa nyimbo zao na kupata umaarufu wanasahau kwamba hii barabara imechongwa na wale legends ambao wanastahili heshima.”
Credit :Timesfm.co.tz

0 comments: