Thursday, May 29, 2014

Nuh Mziwanda asimulia alivyokutana na Shilole

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/03/Nuhu-Mziwanda-akiwa-na-Shilole.jpg
Hakuna asie fahamu kama Nuh Mziwanda na shilole ni wapenzi ,sasa Nuh akifanya mahojiano na kipindi cha Trending Africa cha 100.5 times fm amezungumzia jinsi alivyo kutana na shilole aka shishi mpaka wakawa wapenzi.


Nuh amesema mwanzo walianza kama marafiki lakini kadri siku zilivyo sogea wakajikuta wamezama kwenye mapenzi
"mara ya kwanza kukutana nae ilikuwa studio unajua mimi ni producer pia ,yeye alikuwa tayari kashatoka mimi wimbo wangu wa otea nani ulikuwa unafanya vizuri ,basi tukawa tunawasiliana asipo niuona ananimiss mimi pia nikawa na mmiss lakini mwanzo sikuzani kama angekuwa mpenzi wangu"amesema Nuh


Kuhusu taarifa zilizokuwa zimeenea mwanzo kwamba wanampango wa kufunga ndoa Nuh amesema ni kweli wanamipango huo mungu akibariki watafanya hivyo
Nuh mziwanda ana wimbo mpya unaitwa Msondongoma usikilize hapa..

0 comments: