Thursday, May 01, 2014

BAADA YA DOMAYO NA KAVUMBANGU KUSAJILIWA NA AZAM FC ,YANGA YATOA TAMKO..

Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.

  Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite. 

Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.

Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na  kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu

Uongozi wa Yanga uliandikia TFF  barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.

Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya Azam FC.

 

Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013, alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.

Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.

Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.

Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu ujao.


0 comments: