Tuesday, August 13, 2013

AUDIO:NEY WA MITEGO AMJIBU WALTER CHILAMBO,AZUNGUMZIA LINEX KUKATAA KUPIGA CHORUS''SALAMU ZAO''

Ney

Baada Walter chilambo Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012kupinga  
 tuhuma nzito za Ney wa Mitego kupitia ngoma yake mpya ya ‘salam zao’ ambapo 
kuna lyrics zinasema  
''Hizi Salamu ziende kwa Madam Rita na bongo star search. 
Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?!
Namuona Walter Chilambo kapigika km zamani,
haji ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani,
acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharan'
Walter amesema kuwa maneno haya hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri tu na kwa Ney, Hadhani kama alifanya research kabla hajaimba.

Walter amesema kuwa yeye na Ney hawana ukaribu wowote, na walishawahi kukutana akamuuliza  ni kwanini amemuimba vile katika wimbo wake, Ney alimwambia kuwa 'asipanik' then akapotezea na issue nyingine na kisha kutimua zake.

sasa Ney wa Mitego Exlusive amezungumza na www.SwahiliInfo.blogspot.com na kuzungumzia issue kadhaa ikiwemo habari ya linex kukataa kufanya chorus ya hiyo ngoma kutokana na alichokiimba lakini pia amezungumzia habari zilipo kwenye mitandao ya kuwa ameachana na girlfriend wake

kuhusu walter chilambo ..Ney amesema
‘‘siku moja watakuja kuniambia kwamba asante brother uliongea kitu ambacho labda kimetusaidia ,hicho tu ndo kitu ambacho naweza kumjibu yeye atakuja kuzungumza siku moja ,atakumbuka shuka wakati kumekucha mda mrefu ,hii itawasaidia wasanii wanakuja kupitia Bongo star search’’

kuhusu linex kukataa kufanya chorus..Ney amesema
‘kama mtu alikataa ni shauri yake this is my music,huu ni mziki wangu mimi kama yeye anadai alikataa anasababu zake lakini mimi nimefanya kitu kiko well kiko poa watanzania wanakipokea na wanakikubali kama alikataa may be ni afadhali.’’

Na kuhusu kuachana na Girlfriend wake
‘Minarudia kusema kwamba mimi sijatengana na girlfriend wangu mimi nayeye bado tuko pamoja……………………….
kwa Info zaidi chukua kama dakika tano kumsikiliza Ney hapo chini .

0 comments: