Monday, August 19, 2013

MKOLONI: NIKITAKA KUINGIA KWENYE SIASA NTASEMA.''KWASASA ALBAM INAKUJA''


Kama hujua Mgosi Mkoloni ni mwanachama wa CHADEMA na Alisha wahi kufanya kazi kwa ukaribu na Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'SUGU' (CHADEMA).Sasa swahiliInfo.blog ilitaka kujua kama anampango wowote wa kugombea ngazi yoyote katika siasa..

‘’kila jambo naamini lina wakati wake wa kusema na kutenda ,lakini kwa sasa hivi siwezi kusema kama nataka kugombea hapana ,kwahiyo kikubwa tuombe uhai tuzidi kushirikiana kukiwa na lolote ndo maana kuna vyombo vya habari’

Mgosi mkoloni amesema kwa sasa anatengeneza albam yake wake peke yake na amekwaisha kuachia ngoma mbili ikiwepo ‘’Nyama’’ ambayo amefanya na Juma Nature na mapacha .albam hiyo haijajulikana inatoka lini, ila amewataka fans wake kuwa na subira na kuendelea kumpa ushirikiano..


Kwanini anafafanya kazi zaidi na mapacha na sio Dk John ambaye walikuwa pamoja tangu mwanzo kupitia kundi la Wagosi wa Kaya

‘DK john yupo Tanga mimi nay eye tunaendelea kuna kazi tulifanya inatwa maumivu ya miaka 10 tulimshirikisha chege na kazi zingine tunaendelea kufanya ,anaandika naona naandika tunatumiana wote tupo hatupo tu karibu kuweza kufanya kazi kwa pamoja pamoja kwa sababu tayari kitumbua kishaingia mchanga ,Mapacha ni watu ambao nipo nao karibu  mda mrefu.
Na kuhusu kuvunjika kwa kundi la wagosi wa kaya
Mkoloni amesema ''kundi haliwezi kufa labda sisi ndio tutakufa,kundi lipo na litaendelea kuwepo kazi zitafanyika kila kitu ni mipango na hatuwezi kuacha muziki ,tukiacha muziki inamaana tumeacha mashabiki wote ambao wananisikia saivi ''..
 

0 comments: