Monday, August 12, 2013

Mke WA ZAMANI WA NELSON MANDELA 'WINNIE MANDELA'APINGA MOVIE ILIOFANYWA NA JENNIFER HUDSON..Mke wa zamani  wa rais wa kwanza muafrika nchini afrika kusini Nelson Mandela,
Winnie Mandela,amesema anahisi movie mpya kutoka  Hollywood  ambayo
 imefanywa na muimbaji Jennifer Hudson na star wa filamu  Terrence Howard 
imemkosea heshima .
 
Movie hiyo inaitwa ‘Winnie’ inaelezea story yake Winnie Mandela ,usumbufu 
na matatizo aliyo yapata baada ya mumewe ambaye Ni Nelson Mandela kwenda
jela.
Winnie Mandela amesema film hiyo ni kama imekosa maadili kwani 
uzalishaji wake umefanika ndani ya nchi yake wakati yeye akiwa hai na bila 
kuomba ridhaa yake.
Akizungumza na CNN amesema “
"sina tatizo  na Jennifer,lakini sikubaliani na movie yenyewe  .bado nipo hai
 nazani sio heshima kuja afrika kusini,kutengneza movie kuhusu 
maisha yangu ,na kuita hiyo movie imetafsiri maisha ya mahusiano
 ya Winnie Mandela.nazani imenikosea. 
Star wa  movie hiyo Jennifer Hudson akizungumzia upande wake amesema
 alitaka kuzungumza na Winnie Mandela lakini Producers wa movie hiyo 
wakawa tofauti na mawazo yake .

 

movie hiyo ‘Winnie’ trailer yake tayari imeshatoka ,movie yenyewe  inatarajia kutoka 
rasmi September 6 mwaka huu,utengenezaji wa movie hii ulifanyika Afrika kusini 
kuanzia  2010. 
Winnie bado alikuwa mke wa Nelson Mandela wakati Nelson anakuwa raisi wa 
Afrika kusini May 1994, na taraka ya kutengana kwao ilikamilika rasmi 
19 March 1996.
Lakini licha ya kuachana na Nelson Mandela ,Winnie bado anatambulika kama
'Mother of the Nation'kwa mchango wake wakimapinduzi ya ubaguzi wa rangi
nchini afrika kusini .. 
Tizama  trailer ya  movie hiyo  'Winnie' hapo chini

0 comments: