Wednesday, August 21, 2013

Q-Jay 'ukitaka collabo na mimi ni mpaka roho mtakatifu anipe kibali"

 

Miaka kadhaa iliopita Moja kati ya wasanii waliobalikiwa sauti ya kipekee Q-Jay alitangaza kuachana na Bongo Flava baada ya kuokoka na akasema atakuwa akifanya muziki wa gospel, sasa
SwahiliInfo.blogspot.com exclusive imepiga story na Q –jay na kuzungumzia maisha yake baada ya kuokoka ,muziki wa gospel ,na je anaweza kufanya collabo na msanii wa nyimbo za kidunia ?
Kuhusu maisha yeke mara baada ya uokovu Q-Jay amesema

‘’Kwakweli na mshukuru mungu kwa kuweza kunibadilisha ,ni kwamba mtumikie mungu katika siku za ujana wako,kwahiyo nikitu ambacho kimenijia baada ya kuhubiliwa injili na injili ilipo nichoma nikaamua kumpokea yesu katika maisha yangu ,baada ya kumpokea kristo nilibatizwa nabado naendelea na mafundiso zaidi,kwa hiyo maisha yanaendelea vizuri huku nikiendelea kumtumikia mungu’’

Na kuhusu kufanya muziki wa Gospal..

‘’hiyo nafanya taratibu taratibu kwa nia na makusudi kuweza kuhubiri Injili ya yesu kristo,kwasababu muziki wa injili ni tofauti na muziki wa kidunia huku lazima ujue vizuri neno la mungu’’

Pia SwahiliInfo.blog ilitaka kujua kama Q jay anaweza kufanya collabo na msanii  anaeimba nyimbo za kidunia na hichi ndicho alichojibu

“cha kwanza unafanya maombi, unajua sio kila mtu anataka anishirikishe basi nishirikiane naye  ,kwanza unamuomba mungu akuongoze je ni sawa kufanya na huyo mtu?alafu unapo pata kibari cha roho mtakatifu ndipo unafanya nae..


Kila la kheri Q jay kwa kuamua kumkabidhi mwenyezi mungu maisha yake msikilize hapa...


Tunaomba radhi kwa sauti kuto kusikika vizuri..

0 comments: