Wednesday, August 07, 2013

DIAMOND AKWAMA NCHINI KENYA KUTOKANA NA MOTO JKIA.

 IMG-20130807-WA0019
tukio la moto lililotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA nchini kenya,limesababisha msanii wa bongoflava Diamond kushindwa kurudi bongo kwa wakati akiwa njiani kutokea South Africa aliko enda kufanya video..IMG-20130807-WA0002
hizi ni baadhi ya picha pamoja na ujumbe alioandika kupitia blog ya wasaafi...
Niliwasili Alfajiri ya saa kumi na moja nikitokea nchini South Africa nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi na abiria wengine tukisubiri  kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto. Hadi sasa sasa chanzo cha moto ule uliosababisha kuwaka kwa Airport bado sijajua lakini hii imepelekea safari kukwama,sina uhakika kama tutaweza kuja Dar tena au Ndege kama zitaweza kuruka kwa leo maana hapa tulipo wanatupeleka hotelini. Imewalazimu uongozi wa Immigration kuja na kutugonga mihuri kwenye basi la wasafiri na kuwekewa usalama wa mabegi yetu.
 IMG-20130807-WA0004
IMG-20130807-WA0015

0 comments: