Wednesday, August 07, 2013

MFAHAMU DADA WA DAMU WA MWANASOKA 'CHRISTIAN RONALDO' ANAEFANYA MUZIKI.

 
Dada wa damu wa mwanasoka ghali zaidi duniani Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mnono wa kutengeneza albam yake ya kwanza ya muziki na kampuni ya utayarishaji ambayo hufanya kazi na wasanii wakubwa kama Lady Gaga na J-LO.

Katia Aveiro ambaye single yake ya kwanza "Boom sem parar" imepata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Youtube, tayari ameanza kuunda albam yake na watayarishaji kutoka RedOne huko jijini Madrid - mahala ambapo ndio ameweka makazi yake ya kikazi.

Ronaldo, ambaye jana alipigwa picha akiwa na mwanamuziki J-LO amezungumza kuhusu dili hilo la dada yake na kusema: "Nina furaha sana kwa ajili yake."

 
Aveiro anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha kubwa mwezi ujao jijini Madrid huku albam yake ya kwanza ikitarajiwa kutoka mwezi November. Alisema: "Huu ni mwanzo wa muziki wangu kuwa wa kimataifa." 

0 comments: