Jay Jay Okocha amesaini mkataba wa kuwa balozi wa kinywaji cha Bullet Energy ..
Mwanasoka mkongwe Austin ‘Jay Jay’ Okocha amesaini mkataba wa kuwa balozi wa kinywaji cha Bullet Energy ,mchezaji huyo wa zamani wa Bolton Wanderers FC ameungana na muigizaji wa kike Chika Ike katika dili hilo ambaye sura yake imekuwa kitumika kukitangaza kinywaji hicho .
mkataba wa Okocha na kinywaji hicho unadaiwa kuwa na thamani ya pesa ya Nigeria Naira Million 15 kwa miaka miwili .
Okocha tayari ana dili nyingine ambayo amekwisha kuianza inaitwa ‘Bullet Juggle with JayJay’ ambao mashabiki wa soka wanatuma vipande vya video wakichezea mpira .
Okocha pia alisha wahi kufanya kazi ya kuwa balozi wa kinywaji cha Pepsi na kampuni ya nguo ya Reebok....
0 comments:
Post a Comment