Monday, May 12, 2014

Obama ampongeza mchezaji wa American Football aliejitangaza hadharani kuwa na tabia za ushoga

Obama ampongeza mchezaji wa American Football aliejitangaza hadharani kuwa na tabia za ushoga
Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya American Football (National Footbal League), Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza wa mpira wa miguu kutangaza kuwa anajihusisha na tabia za ushoga.
Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini marekani.


Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake mnamo mwezi february baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo katika chuo cha Missouri ilipongezwa ,huku rais Obama akiwa miongoni mwa watu waliotoa pongezi zao.
Baadhi ya wachambuzi wa michezo walikuwa wamebashiri kwamba baadhi ya timu huenda zikajitenga na umaarufu unaomzunguka mchezaji huyo.
Credit :times fm

0 comments: