Thursday, May 15, 2014

SAUTI:Makamua kulipwa pesa baada ya wimbo wake kuchezwa kwenye Radio za Sweden..

 
Makamua amesema wimbo alio mshirikisha Saraha Don’t cry unafanya vizuri nchini Sweden na huenda hivi karibuni akaanza kupokea malipo kutokana na wimbo huo kuchezwa kwenye vituo vya radio nchini humo.

 
Makamua akifanya mahojiano na kipindi cha Times Fm (Trending Afrika )amesema hivi karibuni aliwasiliana na saraha ambaye ni raia wa sweden na kuzungumzia kuhusu mpango wake wakutaka kuuweka wimbo huo kwenye albam yake ,wimbo ambao umeshaanza kuchezwa kwenye Radio za nchi hiyo.

 “Few months ago saraha alinitafuta kwa njia ya mtandao akaniambia tunaweza tukatumia don’t cry kwenye albam yangu ?nikamwambia why Not ,fresh kwasababu pia utaitangaza bongo flava Sweden na hiyo itasaidia kwasababu ni more than featuring tumefanya Duet akaniambia na ngoma itaenda sawa ,kwahiyo aliitoa nyimbo imefanya vizuri Sweden nazani ntaanza kulipwa kutokana na inavyo rotate kwenye air wave za Sweden yeye atakuwa huku mwezi wa saba nazani ataweza kuongea vitu vingi kuhusu hilo “ amsema Makamua

Msikilize hapa…

0 comments: