Wednesday, May 14, 2014

Diamond Platnumz atajwa kuwania tuzo za Bet 2014

Diamond (2)

Baada ya kunyakua tuzo 7 za KTMA 2014, na kuwa nominated katika tuzo za MTV ‘MAMA’ nchini Afrika Kusini, sasa Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo kubwa zaidi za kimataifa BET Awards za nchini Marekani.


 Hit single yake ya ‘Number 1’  ndio iliyompa tiketi Diamond kuwa nominated katika kipengele cha ‘Best International Act: Africa’, ambapo anachuana na mastaa wengine wa Africa ambao ni Davido(Nigeria),  Mafikizolo (Afrika Kusini),  Sarkodie (Ghana), na Tiwa Savage (Nigeria).

Diamond ndiye msanii pekee wa Afrika mashariki katika tuzo hizo.
Hivi ndivyo ilivyoandikwa katika mtandao wa www.bet.com

BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA NUMBER ONE& (TANZANIA)
TANZANIAN STAR DIAMOND PLATNUMZ BECAME A GLOBAL FORCE WITH SUCCESS OF HIS HIT NUMBER ONE AND THAT WAVE MAY CONTINUE WITH A WIN FOR BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA

Sherehe za ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika June 29 huko Los Angeles, Marekani
Tuzo za BET huandaliwa na kituo cha TV cha Black Entertainment Television, na zilianzishwa mwaka 2001 kusheherekea mafanikio ya kazi za   Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo na maeneo mengine ya burudani.

Hongera sana Diamond Platnumz, endelea kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

0 comments: