Monday, May 19, 2014

Cyrill asema ugumu wa taratibu za kutunza Camera za kuazima nje ya nchi ni kikwazo, kushuti 'Alowa' na director wa Kenya


Cyrill asema ugumu wa taratibu za kutunza Camera za kuazima nje ya nchi ni kikwazo, kushuti


Ubora wa video ni moja kati ya hatua kubwa wanayoifanyia kazi wasanii wengi wa Tanzania ili video hizo zinapoifunika audio nzuri wanazofanya zikubalike katika vituo vikubwa vya runinga vya kimataifa.
Wapo wasanii kadhaa ambao kwa kutumia waongozaji wa Tanzania video zao zimeweza kuchezwa MTV na Channel O.

 
Cyril Kamikaze ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Alowa’ wiki kadhaa zilizopita ni mmoja kati ya wasanii wanaotamani kufanya video bora zaidi kwa kutumia waendeshaji wa Tanzania na amekuwa akiwaza kukodi vifaa bora zaidi kutoka nje ya nchi lakini taratibu za kuvitunza vimekuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wake.
Cyril ameeleza kikwazo hicho kupitia kipindi cha Trending Africa wakati anafanya mahojiano na watangazaji wa kipindi hicho, Julian Ishungisa aka Jayree na John aka Jonijo.
“Actually we have good directors kiukweli tuna madirector wazuri sana. Lakini at the end of the day tunajaribu kuangalia utofauti. Probably pia kuna vifaa unajua, sometimes unataka kufanya video unaona ‘aah kuna camera fulani haipo’. Nikitaka ile camera ije ili nipate ile quality, like..tuiagize. camera inatakiwa ije na walinzi sijui…ilale polisi. Kuna mambo mengi yanakuwepo katikati.” Amesema Cyril.
Rapper huyo ameeleza kuwa kutokana na ugumu huo huamua kuwafuata watayarishaji wa nchi za jirani na kwamba video ya wimbo wake ‘Alowa’ atafanya na muongozaji wa Kenya ‘Enos olik ambaye ameongoza video nyingi nzuri kama ‘Gere’ ya Weusi na Kioo ya Jaguar.
Kipindi cha Trending Africa kinakuwa hewani kupitia 100.5 Times Fm na huongozwa na Julian Ishungisa aka Jayree na John aka Jonijo.
Credit :Timesfm

0 comments: