Monday, May 19, 2014

Lupita Nyong'o anatarajia kucheza kama mfanyakazi wa ndani kwenye movie mpya ' Southpaw’

lupita
Mshindi wa tuzo za Oscar Muigizaaji wa kike kutoka nchini kenya Lupita Nyong'o ambaye amjipatia umaharufu mkubwa kupitia filamu ya '12 years a slave' anatarajia kuendeleza makali yake katika filamu mpya inaitwa  ' Southpaw’.


Filamu hiyo inamuhusu bondia anaepambana kurudisha ubora wake baada ya kufulia, ndipo Lupita anajikuta anahusishwa na maisha ya bondia huyo ambaye alikuwa akimfanyia kazi ya kumlea mwanae wa kike.
washiriki wengine wa filamu hiyo ni pamoja na Rapper Eminem, Jake Gyllenhaal, Forest Whitaker, Rachel McAdams na wengine wengi ,tarehe ya kutoka kwa filamu hiyo haijajulikana .
Taarifa zingine zinasema muigizaji huyo wa  ‘12 Years a Slave’anatarajia kuigiza katika filamu zingine mbili   ‘A Most Wanted Man’ na ’Taken’...

0 comments: