Tuesday, May 27, 2014

MAYWEATHER AMUOMBA RADHI MKE WA T.I NA WANAE KWA UGOMVI KATI YAKE NA T.I NA KUMUITA ‘KAHABA’


 
Bondia Floyd Mayweather amemuomba radhi mke wa T.I, Tiny kufuatia ugomvi kati yake na T.I ambao ulipelekea yeye kumtaja kwa jina la kumdhalilisha ‘kahaha’.


Mayweather amemuomba radhi Tiny kupitia mtandao wa NecoleBithie na kueleza kuwa mke wa T.I hajawahi kumkosea heshima.
“Only person I wanna apologize towards is Tiny. She cool. She never been disrespectful to me.” Amesema Mayweather.
Bondia huyo aliwaomba radhi pia watoto wa T.I na watoto wa Tiny.

Mayweather na T.I waliingia katika ugomvi uliopelekea kurushiana vipi baada ya T.I kumfuata bondia huyo na kumuzishia vurugu. T.I alikasirishwa na kitendo cha Maywather kuonekana mara kwa mara na mkewe na kupost picha kwenye mitandao.
Hata hivyo, Mayweather ameeleza kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tiny na kwamba alimfahamu hata kabla hajamfahamu T.I na kwamba rafiki yake Tiny ndiye aliomba kwenda kwenye pambano lake na akaja na Tiny.

0 comments: