Tuesday, May 20, 2014

50 cent akasirishwa na kuto kualikwa katika mahafali ya mwanae akimaliza high school.

Kufuatia kuenea kwa habari za 50 kuto kuhudhuria mahafali ya mwanae wa kwanza wa kiume Marquise akimaliza high school mwinyoni mwa wiki na kupelekea watu kumsema vibaya jamaa amelazimika kutolea ufafanuzi swala hilo ambapo kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilicho zungumza na TMZ kimesema 50 hakufika katika mahafali hayo kutokana na kuto kualikwa wala kujua wapi yalikuwa yakifanyika

Chanzo hicho kimeendelea kusema 50 aliumia baada ya kuone picha za mahafali hayo kwenye mitandao na kama angepata mualiko basi angefika.

Jumamosi iliopita Marquise alimaliza High School pasipo 50 cent kuhudhuria mahafali hayo na kisha picha nyingi kuenea kwenye mtandao wa facebook zikimuonesha Marquise akiwa na dada yake pamoja na mama yake.

Hapo mwanzo kulikuwepo na taarifa za Marquise kumchana 50 ambaye ni baba yake kupitia Facebook kwa madai hamjali.

0 comments: