Wednesday, July 02, 2014

Grandpa Records yatoa tamko baada ya DNA kujitoa katika label hiyo..

dna
Baada ya rapper DNA kutoka nchini Kenya kutangaza kuachana na Lebel iliokuwa inamsimamia Grandpa Records akidai anataka kufanya kazi zake kwa kujitegemea lebel hiyo imetoa tamko kuhusu kilicho sababisha jamaa kuondoka.

"GrandPa Records/GrandPa Government imekuwa ikikuwa na kusimamia wasanii wenye majina barani africa,DNA alikuwa nisehemu ya familia yetu ,tumehusika kwenye mafanikio yake makubwa baada ya kurudi kwenye game mafanikio ambayo hayajawi kutokea katika msanii wa afrika mashariki na tumekuwa pamoja katika miaka miwili ambayo tumefanya kazi pamoja ,ni msanii mwenye kipaji.
mkataba wake na  Grandpa Records umeisha may 2014 kwa makubaliano ya pande zote mkataba wake hauto ongezwa na amemaliza mkataba wake vizuri hakuna tofauti kati yake na Grandpa records.
GrandPa Records,artists,producers na wafanyakazi wote tunamtakia heri dennis waweru kaggia a.k.a DNA katika kazi zake.
Aidha taarifa hiyo imesema Grandpa Records itaachia nyimbo za DNA zilizobakia kwa makubaliano kati yeo na DNA.

0 comments: