Msanii wa Nigeria, Davido anaendelea kusaka nafasi ya kuwa
kati ya wasanii wakubwa zaidi sio tu Afrika bali dunia nzima kwa ujumla. Siku kadhaa baada ya kutangaza collabo na Meek Mill na Rick Ross,
mwimbaji huyo wa ‘Aye’ ameiambia Encomium kuwa yuko katika mazungumzo na
rapper wa Young Money, Drake kwa ajili ya kufanya collabo kwa usimamizi
wa Don Jazzy.