Tuesday, October 07, 2014

Linah aweka wazi gharama alio tumia ktengeneza video ya Ole Thamba.


Msanii wa kike hapa nchini Linah amesema alitoa shilingi milioni 49,800,000 na kumkabidhi muongozaji wa video wa Afrika Kusini, Godfather kushoot video ya Ole Themba.

“Godfather tulimkabidhi $15,000 mbele ya mashahidi na baada ya hapo tukamalizia tena dola $15,000 jumla ikawa $30,000 na mikataba tunayo kwa anayebisha, amesema Linah.Unajua wanachukulia vitu rahisi rahisi, kwenye ile video kuna vitu kama ile gari ambayo Godfather alidai haikuwahi kutumia kwenye video za Afrika Mashariki, kuilipa ile kampuni ya model. Sema tulijitoa ili kufanya hivyo ili kupata kitu kizuri. Hata mimi wakati nakabidhi hiyo pesa roho ilikuwa inauma sana.”

0 comments: