Monday, February 04, 2013

Msanii wa BongoFlava BUIBUI Agongwa na kuvunjika miguu..

 habari isiyo nzuri iliyopo hivi sasa ni kumuhusu msanii  Frank Ktende a.k.a Buibui, ambae amepata ajali weekend hii, kwa kugongwa na boda boda maeneo ya Kinondoni studio, na kusababisha mguu wake wa kushoto kuvunjika na mguu wa kulia kuteguka 
Kisa cha mpaka kufikia kugongwa na pikipiki hiyo, ni pale alipokuwa na washkaji zake na mwanadada mmoja alimtaja kwa jina la Lina J, ambae ni mschana anaefanya nae video ya wimbo wake, video  iliyokuwa inataki kukamilika siku ya jana.  
 
"yule msichana nikamwambia kama vipi huu muda umeenda sana, mida ya saa saba saa nane, turudi tu home  tukapumzike kwasababu kesho tena tunamalizia hii video,huku na huku tukaondoka, lakini katika wale vijana tuliokuwanao, mmoja simfaham ila mwingine namfahamu, sasa huyo mshakaji alikua anamtaka huyo msichana, mi sijawahi kumtongoza, kwasababu namchukulia kama dada yangu nae ananichukulia kama kaka yake , na mimi sikupenda kwasababu yule sio malaya, nikaona bora nimrudishe yeye kwanza halafu na mi ndio nirudi  kulala kinondoni. 
 kumshusha yule,  sasa yule jamaa alikua kakaa mbele akawa kama amemaindi hivi, kwanini buibui kakubali tumrudishe huyu  kwanza, kwanini asituache nae, kwasababu alikua anafosi wanishushe mi kwanza halafu wao waendelee nae safari yao, sasa yule dada akaniambia "Buibui, nipeleke mimi kwanza huwezi juwa naweza nikafanyiwa kitu kibaya" kumrudisha akashuka wakawa wananirudisha mimi Kinondoni, basi kufika studio mi nikashuka lakini yule jamaa alikua kalewa akaanza kutoa shit huna lolote, nikashuka, nikawa natembea, sa wakati natembea kuna mshkaji akanambia mbona huyo jamaa ameshika jiwe kwa nia ya kukupiga, sa mi nikageuka kuangalia mshkaji gani huyu anaetaka kunipiga, wale wa bajaji kwasababu wananijua wakamuwahi , sa ile nageuka kushoto kwangu, narudi kuangalia kulia kwangu, nakutana na pikipiki na moto ikanigonga, lakini nilikua kwenye service road."


0 comments: