Wednesday, February 26, 2014

Exclusive:PNC asema sijadhalilishwaji ila sikujua kama narekodiwa na kupigwa picha.(audio)Baada ya kuenea kwa picha na video inayomuonesha PNC akiwa amepiga magoti akimuomba msamaa ustadhi juma na musoma ili aendelee kumsimamia kazi zake na wengi kutafsiri picha hizo kama ni udharirishwaji kwa msanii PNC,SwahiliInFoBlog imepiga story na PNC kujua mtizamo wake,


PNC amesema kila mmoja anaongea la kwake kuhusu hizo picha lakini yeye anaona ni sawa kwani maneno huja na kusahalika ilimradi kazi zake zinzendelea 


Je alikuwa anajua kama anarecodiwa na kupigwa picha ?


“Mimi sikujua chochote tulikuwa tupo pale kama watu watatu hivi ,kuna mmoja ndo alikuwa anapiga picha  sijui ndo aliambiwa arekodi au laah sijaelewa chochote lakini mi mwenyewe nimeshangaa nimekuja kuona hivyo kwenye mtandao ,lakini poa kwasababu mimi nilikuwa na mwambia nam-please naomba msamaa lakini mimi sijaona hatari yoyote wa hizo picha, kuomba msamaa sio ujinga ni kitu cha kawaida”


Je baada ya kuomba msamaa umesamehewa ?


“Amenisamehe mimi naamini amenisamehe kwasababu nimeshaanza na project nyingine kwa Mazuu amenilipia pale”

Msikilize hapo chini

0 comments: