Wednesday, May 29, 2013

AUDIO:IZZO B azungumzia Kifo cha Ngwea , Ashindwa kujizua amwaga chozi...

Habari za kusikitisha katika mziki wa bongo flava ni kifo cha rapper albet mangwer kutoka east zoo ambaye amefariki jana nchini africa kusini,sababu za kifo chake bado hazijajulikana japo kuna habari huenda kikawa kimesababishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya kupita kiasi ,
kwa mujibu ya watanzania walio afrika kusini ambao ndio walikuwa wenyeji wa ngwea wanasema jamaa alilala usiku wa juzi baada ya kupiga kama show mbili ivi nchini humo  na jana alitakiwa asafiri kurudi bongo lakini walipo enda kumgongea alipolala hakuweza kuamka mpaka alipo pelekwa hospital na kujuliakan amefariki dunia.
 **************************************************

Kutokana na kifo chake wasanii wengi wameguswa na kifo hicho na na kupelekea baadhi yao kuairisha show zao za mwishoni mwa wiki mmoja wao ni rafiki mkubwa wa marehemu Tid pamoja na kikosi cha mizinga na mwana fA Ambaye ameshawahi kufanya kazi na ngwea.
mwingine ni izo b ambaye alikuwa na show yake jijini mbaya ila kwa heshima ya ngwea ameairisha show hiyo ,izzo akipiga story na SwahiliInfo amesemaNgwea anamchango mkubwa katika mziki wake kwani albam yake ya kwanza ya bongo flava kuinunua ilikuwa ya Ngwea AkA MiMi kipindi hicho Akiwa Form Two..
Msikilize izo akizungumzia alizipata vip taarifa hizi za msioba na jinsi alivyo amua kuairisha show yake
kwa mujubu wa msemaji wa familia ya Mangwea msanii huyo anatarajia kuzikwa morogoro maahara ambapo ipo familia yake na  ndiko alikozikwa baba yake mpaka sasa haijajulikana mwili wa marehem utafika lini hapa dar kutokea afrika kusini lakini watanzania walioko huko wanafanya utaratibu na ubalozi wa tanzania nchini huo ili kufanikisha swala hilo.
Rest in Peace Albet Mangwea.

0 comments: