Friday, May 31, 2013

RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEA KUTOKA KWA KAKA WA MAREHEMU KENNETH ..

Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumamosi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini, ukitokea nchini Afrika ya kusini.Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, 

  Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa viwanja vya leaders club na kampuni itakayoshughulikia zoezi hili ni Entertainment Masters na baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.
Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo laKihonda, mkoani,Morogoro...!!

 

0 comments: