Friday, May 10, 2013

Jay Z na mpango wa kumsaini mwanasoka Neymar ,Roc Nation Sports.

Siku chache baada ya Rapper  Jay Z kufungua kampuni ya uwakala wa wanamichezo Roc Nation sports, taarifa zilizoendea kwenye mitandao ni kwamba rapper huyo anajipanga kumsaini mshambuliaji wa Brazil Neymar kwenye kampuni hiyo .

“Roc Nation” iinataka kujikita katika michezo yote hasa soka, ikijaribu kuwafanya wachezaji kuwa mastaa wa kweli duniani kwa kuwa na mikataba minono na makampuni tofauti. Ndio maana Neymar kwa sasa amepewa kipaumbele kuwa mcheza soka wa kwanza kusainiwa kwenye kampuni ya Jay Z."

Neymar ataungana na Robinson Cano wa New York Yankees na Skylar Diggins wa WNBA katika listi ya wanamichezo waliopo katika kampuni ya ya Jigga inayoanza kukua kwa kasi japo imeanzishwa mapema mwaka huu.
Katika ripoti nyingine inasemekana Jay Z pia amekuwa katika mawindo ya kuwasaini wabrazil wengine Lucas Moura na Leandro Damião, pia Jon Jones, bingwa wa sasa ndondi uzito mwepesi wa UFC.
Lakini Jay Z atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa kampuni ya masoko ya michezo inayomilikiwa na gwiji wa Brazil Ronaldo, ambayo ilimsaini Neymar kumwakilisha katika haki zake za taswira yake mwaka 2011.


0 comments: