Monday, June 24, 2013

Waafrika wanaofanya vizuri katika ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA ....

Kuna historia ndefu kwa wachezaji kutoka afrika kuweza kujitengezea jina wenyewe katika ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu NBA.


Nchi ya Nigeria ndio inayoongoza kwa kuwa na wachezaji wengi katika ligi ya NBA hadi sasa,

Orodha hii inahusisha wachezaji ambao wanacheza kwa sasa katika timu mbalimbali ndani ya ligi hiyo ya NBA.

Hasheem Thabeet

Taifa: Tanzanian

Urefu: 7 ft 3 in

Thabeet siyo mgeni katika mchezo huu wa kikapu ingawa ameingia akiwa amechelewa, ameanza kukiendeleza kipaji chake baada ya kuwa kuanza kuangalia mashindano mbalimbali jijini Dar es Salaam. Amehudhuria katika Chuo Kikuu cha Connecticut. Mwaka 2008 na 2009 amewahi kutajwa kuwa mchezaji wa mwaka na NABC kama mlinzi bora wa mwaka.
 Ni mtanzania wa kwanza kucheza katika lihi hii ya NBA kutajwa kuchezea timu ya Memphis Grizzlies mwaka 2009. Baadaye akachezea timu za Houston Rockets na Portland Trail Blazers kabla hajaenda katika timu ya sasa ya Oklahoma City Thunder. Thabeet ni mchezaji mrefu zaidi katika wachezaji wa NBA. Mwezi November mwaka huu Thabeet ameweka rekodi yake ya kwanza katika mchezo huo kwa double-double akiwa na pointi 13 na rebound 10.

Festus Ezeli

Taifa: Nigeria

Urefu: 6 ft 11 in

Ezeli ametumia muda wake mwingi wa utotoni katika masomo akiwa kwao nchini Nigeria. Ni baada ya kuanza kuishi na mjomba wake nchini Marekani ndipo alipoanza kucheza kikapu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 14. Mara ya kwanza kuingia katika mchezo ilikuwa ni kama ajali baada ya kutofahamu na kujikuta akifunga katika goli lake. Ni mwaka 2006 ambapo mwishowe alianza kukaa vizuri katika mchezo huo na mwezi July mwaka 2007 alipata mwaliko kutoka Reebok All-American Camp.
 Wakati huo alikuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt kwa miaka mitatu kabla hajakuwa nyota katika mchezo huo wa kikapu, akiwa na wastani wa pointi 13 na rebound 6.3. msimu huo aliyajwa kuwa namba mbili katika timu ya All-SEC (Southeastern Conference). Kwa sasa anakipiga katika timu ya The Golden State Warriors akiwa na umri wa miaka 23 na amesajiliwa na timu hiyo mwaka huu wa 2012.

DeSagana Diop

Taifa: Senegal

Urefu: 7 ft 0 in

Diop amekulia nchini kwao Senegal, ambako alikuwa anapenda kucheza mpira wa miguu. Ameanza kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 15. Alijiunga na masomo ya sekondari katika shule iliyoitwa Oak Hill Academy mjini Virginia, ambako alikuwa anawaongoza kwa kushika namba moja katika orodha ya taifa. Diop alitajwa kujiunga na timu ya Cleveland Cavaliers moja kwa moja akitokea shuleni. 
Amedumu kwa misimu minne akiwa na timu ya Cleveland kabla ya kutimkia timu ya Dallas Mavericks, New Jersey Nets kisha Charlotte Bobcats mwaka 2009 ambako anakipiga hadi sasa. Diop, ambaye ana uwezo wa kuzungumza lugha tano, ni muislamu. Ana akaunti katika mtandao wa mawasiliano ya kijamii wa twitter ambao huutumia kuelezea kuhusu maisha yake hasa watoto wake.

Al-Farouq Aminu

Taifa: America/Nigeria (huiwakilisha nchi ya Nigeria katika mashindano ya kimataifa)

Urefu: 6 ft 9 in

Aminu amepata elimu yake katika shule ya Norcross High School, Georgia shule ambayo hujulikana zaidi kuzalisha wanamichezo. Kibongo bongo hapo ni Makongo. Alikuwa anaiongoza timu ya shule katika kushinda mashindano mbalimbali na amewahi kucheza katika timu ya McDonald's All-American Team. Akiwa chuo alikuwa anachezea Wake Forest. 
Wakati akiwa chuoni mwaka 2009 alikuwa katika timu ya Sporting News All-Freshman. Mwaka 2010 alikuwa chaguo la nane la timu ya LA Clippers. Mwaka 2011 aliuzwa katika timu ya New Orleans Hornets ambako anacheza hadi sasa. Ameichezea timu ya taifa ya Nigeria katika mashindano ya Olympic mwaka 2012.

Bismack Biyombo

Taifa: Congo

Urefu: 6 ft 9 in

Biyombo amegundulika katika mashindano ya vijana yaliyofanyika nchini Yemen wakati huo akiwa na umri wa miaka 16. Ugunduzi wa kipaji chake ukamuongoza kucheza na mhispania Illescas, ambapo aliitwa kuchezea timu ya wakubwa. 
Akadhihirisha kuwa ni mchezaji wa kimataifa kwa timu ya Fuenlabrada. Biyombo aliufanya ulimwengu wote kumtupia macho hasa wale wanaotafuta wachezaji baada ya kuweka rekodi ya kwanza katika kikapu ya triple double (akiwa na pointi 12, rebound 11 na block 10) katika mashindano ya 2011 Nike Hoops Summit. Baadaye mwaka huo huo wa 2011 alichaguliwa kuichezea timu ya Sacramento Kings, lakini akauzwa kwenda timu ya Charlotte Bobcats, ambako anakipiga hadi sasa.

Christian Eyenga

Taifa: Congo

Urefu: 6 ft 7 in

Eyenega alianza kuichezea timu ya kikapu ya nyumbani kwao Congo katika timu ya Onatra Kinshasa. Na haichukua muda mrefu akatimkia nchini Hispania wakati huo akiwa na umri wa miaka 17 na akafanikiwa kujiunga na timu ya DKV Joventut. Baadaye Eyenga akabounce kati ya timu ya Prat na DKV Joventut. Mwaka 2010 aliichezea timu ya Cleveland Cavaliers, mara ya kwanza katika ligi kuu ya NBA kasha akafanya mkataba wa miaka miwili uliokuwa na thamani ya dola 2 million. 

0 comments: