Monday, December 23, 2013

Vin Diesel atangaza tarehe ya kutoka kwa Fast and Furious 7

Vin Diesel atangaza tarehe ya kutoka kwa Fast and Furious 7
Muigizaji mkuu wa filamu ya Fast and Furious, Vin Diesel ametangaza tarehe ya kutoka kwa muendelezo wa saba wa filamu hiyo yenye mafanikio makubwa. Kutoka kwa filamu hiyo kuliathiriwa na kifo cha aliyekuwa muigizaji mwingine wa Fast and Furious, Paul Walker mwishoni mwa mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

 
Kupitia Facebook, Diesel ameweka picha akiwa na Paul Walker na kuandika kuwa hiyo ilikuwa scene ya mwisho kuwa na staa huyo na kutangaza rasmi kuwa Fast and Furious 7 itatoka April 10 mwaka 2015.
“The last scene we filmed together…
There was a unique sense of completion, of pride we shared… in the film we were now completing… the magic captured… and, in just how far we've come… Fast and Furious 7 will be released… April 10th 2015! P.s. He'd want you to know first…,” ameandika Diesel.
Hakuna taarifa nyingine iliyotolewa kuhusiana na utayarishaji huo utakavyoendelea bila kuwepo kwa Paul Walker.
source .timesfm.co.tz

0 comments: