Hi All, TATIZO = FURSA
> Wasanii wengi kwa kipindi kirefu tumekuwa tunalalamika kuwa
tunabaniwa kwenye MEDIA bila kuelewa kwa kifupi tu ukweli wa mambo. Kwa
Uchunguzi nilioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu hivi nimegundua haya,
Watayarishaji au watangazaji wa vipindi kwa siku wanapokea zaidi ya
nyimbo 30 kutoka kwenye studio mbalimbali hapa nchini, kwao inakuwa ni
vigumu kucheza nyimbo zote kutokana either muda kuwa mdogo wa vipindi
vyao au kuwa na request nyingi za nyimbo ambazo wamekuwa wanazicheza
sana.
> Swali likaja kwangu nyimbo au video ambazo hazichezwi na ni nzuri
tufanye nazo nini ili na hawa wasanii wapate airtime?
>