Monday, June 02, 2014

Chris Brown aachiwa huru baada ya kukaa jela siku 108


Mwimbaji wa R&B, Chris Brown ameachiwa huru baada ya kutumikia kukaa jela kwa siku 108 kati ya siku 131 alizokuwa amepangiwa na mahakama hapo awali.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mkali huyo wa ‘Loyal’ ameachiwa huru majira ya usiku wa manane kuamkia leo.


Awali mwimbaji huyo alihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha mwaka mmoja lakini jaji alimpunguzia siku 116 alizokuwa amekaa rehab na siku 59 alizokaa rumande hivyo alitakiwa akae jela siku 131.
Chris Brown alihukumiwa kifungo hichgo baada ya kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio (probation) aliyopewa kutokana na kesi ya kumpiga Rihanna mwaka 2009.
Hata hivyo, bado yuko kwenye hatihati ya kurudi tena jela kwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtu mmoja huko Washington DC ambayo inatarajiwa kusikilizwa miezi michache ijayo.
Chris Brown amepost kwenye twitter ujumbe baada ya kutoka jela.

0 comments: