Wednesday, June 04, 2014

Mtoto wa kike wa R.kelly ajitambulisha kama mwanaume.

 Jay Kelly
Wakati mataifa mengi ya afrika yakipinga vitendo vya usagaji na ushoga na kuyaacha mataifa ya ulaya na marekani kuendelea kuunga mkono vitendo hivyo,mtoto wa kike wa muimbaji nguli wa muziki wa R&B duniani R.Kelly anayeitwa  Jaya amejitambulisha kama Dume Jike “transguy” kupitia mitandao ya kijamii. 


Transguy ni msichana aliejibadili jinsia kisayansi na kuwa mwanaume  ,Jaya,ambaye anajiita  Jay ameonekana katika picha zake alizoweka kwenye mitandao akiwa amevalia kama mwanaume na kuonesha tabia za kiume.
mama yake Jay ,Andrea Kellyambaye hufanya kipindi kinachoonesha uhalisia reality TV show (Hollywood Exes), ameonesha kukubaliana na hali aliyonayo binti yake ,haijajulikana R.Kelly anajisikiaje kwa kuwa hayupo karibu sana na mwanae
kama ni kweli mtoto huyo wa kike wa R.Kelly anampango wa kwenda kubadili jinsia atakutana na wakati mgumu kwani hospital nyingi m,arekani zilizokuwa zikifanya hivyo zimefungwa .

0 comments: